JINSI
YA KUWEKA FILE TOFAUTI TOFAUTI KWENYE BLOGGER
CLASS
1
Audio fIles
Changamoto kubwa inakuja pale ambapo mtu haelewi namna
gani ya kufanya ili kuweka kitu chake kwenye blog yake na pia wengine huwa
wametengeneza PDF files, Audio files, Video Files na kadha wa kadha, lakini
shida inakuja namna gani wafanye ili kuweka
kwenye blog yao.
Habari njema ni kwamba kitu chochote kinawezekana
kuwekwa kwenye blog na unaweza kukipost na watu wakakiona au hata kukidownload.
Ni rahisi sana kwani hakuna jambo lisilowezekana chini ya jua.
Techno Online Riches tupo hapa ili kukusaidia kupiga
hatua katika topic hii ya namna rahisi za kupost kitu ulichokiandaa nje ya blog
kwenye blog yako hususani blogger.com.
Hatua
za kufuata:
Kuna hatua kadha wa kadha ambazo unatakiwa kuzifuata
ili kwamba uweze kufanikiwa swala la kupost files kwenye blog yako na hatua
hizo zipo za ujumla na pia zipo za mgawanyiko kulingana na aina ya file
unayotaka kuiapload.
Kwa kuanza na AUDIO FILE zifuatazo ni hatua za kupost
audio file kwenye blog yako
AUDIO
FILE (Mp3,Wave, m4a etc)
1.
Hakikisha
umeziweka audio file zako zote kwenye google driver.
Kwanini file hizi uziweke kwenye google
driver, google driver store huwa inatoa link ambayo ukiituma kwa mtu yeyote
anaweza kuona kitu kile ulichokituma na hii inafanya urahisi wa file lako la
audio kuwa na uwezekano wa kuonekana kwa mtu yeyote ambaye analink ya wimbo huo
na kuusikiliza hata kuudownload. Google drive inahusika kuhifadhi file za aina
zote unazozifahamu, yaani Docs, Videos, Audios, Pdf, excel, Images, Setups n.k
zote hizi huweza kuhifadhiwa kwenye google drive na hurahisisha namna ya
kushare na marafiki au dunia nzima kile kitu ulicho kihifadhi huko.
Kama hujui namna ya kuweka File zako
kwenye google drive basi utaangalia video ya namana ya kuhifadhi vitu kwenye
google drive hapa chini
Baada ya kuweka File lako la audio
kwenye Google Drive basi fuata hatua inayofuata.
2.
Tengeneza
post kwenye blogger
Ndio kama Audio unayotaka kuweka ni
file inayojitgemea au inamaelezo Fulani basi usiogope, tengeneza post kwa
kubonyeza NEW POST kisha andika Title ya Audio yako kwenye Title channel, kisha
ingia kwenye uwanja wa kuandikia post
Zingatia yafuatayo, Audio file tunayoenda
kuiweka haitakiwi kuonekana kama Link isipokuwa link tutakayoikopi ionekane
katika mfumo halisi wa audio yaani ionekane kama Mziki kamili ambao mtu anaweza
kuuplay, kudownload na n.k kwahiyo kwenye uwanja wa kuandikia post hapo
hapaleti uhakisia wa audio isipokuwa panleta mfumo wa link tu, kwanini
unafikili?
Blogger inatoa mifumo miwili kwenye
uwekaji wa post zako ambayo ni
1.
HTML
VIEW
2.
COMPOSE
VIEW
Mfumo
unaotangulia pindi tu utakapoingia kwenye sehemu ya kutengeneza post ni COMPOSE
VIEW ambao huu unaonyesha kile unachotaka kukiandika direct kwenye blog yako
kama post, na hapa hutumika sana katika post unazozitengenezea ndani ya blogger.com
yenyewe.
HTML VIEW
Hapa
ni mahali ambapo panahusiana na Code ambazo ndizo zinazotumika kisha
hubadilishwa kuwa kitu halisi kinachoonekana, Html Vie ni sehemu pekee ambayo
inatumika kugeuza link kuwa kitu halisi kinachoonekana, kwahiyo hii eneo
linahusika kuonyesha vizuri nini unachoenda kuweka kwenye blog yako.
Kwahiyo
chagu sehemu iloandikwa HTML VIEW ambay inapatikana mkono wa kushoto juu karibu
na mishale ya back and fore, hapo kuna alama ipo inayoonyesha kushuka chini
bonyeza hiyo kisha utaona chaguo hizo mbili, baada ya kubonyeza, basi fuata
maelekezo ambayo ni hatua ya 3
3.
Nenda
kwenye Google drive kisha copy link ya audio file yako
Baada
ya kufungua html view basi utatakiwa kurudi kwenye google drive ili ukachukue
link ya file amabayo unataka kuipost kwenye blog yako. Chakufanya ni
i.
Nenda kwenye audio file yako kisha right
click ili upate option ya hiyo audio
ii.
Chagua Get link
iii.
Kisha ingia sehemu imeandikwa restricted
na badilisha hapo iwe “anyone with the link”
iv.
Kisha bonyeza copy link na link itakuwa
copied kwenye clipboard.
Hapa utakuwa tayari
umekopi link na sasa turudi kwenye Blogger post channel, pale tulipokuwa
tumefikia kwenye hatua namba 2
4. Baada
ya kukopy link unachotakiwa kufanya ni kufuata maelekezo haya kwa urahisi sana
utachagua either kuandika mwenyewe au kukopy hii HTML kisha upaste kwenye
account yako, chaguo ni lako. Lakini kumbuka system language ni English codes.
Twende pamoja
Ukishafungua
pale pa HTML anza na alama zifuatazo
Copy
this Html or follow only insturctions
<iframe
src=‘the audio file link/’
kwenyelink utakuta neno View badilisha hilo neon kuwa Preview
width=‘100%’
frameboarder= ‘0’
>/
Kisha
bonyeza publish na ubonyeze Comfirm na hapo audio yako tayari umeipost na mtu
ataweza kuisikiliza vizuri.
Kumbuka:
Hii
ni HTML ambayo inawezesha kuweka audio kwenye blog lakini audio hiyo haitakuwa
na selection ya kudownload isipokuwa mtu ataweza kuisikiliza tu pasipo
kuidownload.
Ili
hiyo audio idownloadiwe, basi fuata maelekezo ya HTML hii inayofuata hapa chini
HTML FOR AUDIO DOWNLOAD
OPTION
Mahali
hapa unaenda kujifunza namna ya kufanya hiyo audio file iweze kudownloadiwa na
mtu yeyote na kuisikiliza pia, fuata maelekezo na ufanye kwa uweledi sana
mahali hapa, ni rahisi pia usiogope, kuna html ambayo nitaiweka pia utaiweza
kuicopy na kuitumia kwenye kazi yako ya kuweka audio file kwenye account yako.
Twende
sambamba
<
audio controls>
<
source src= ‘ AUDIO LINK usisahau kubadili neon VIEW kuwa preview ‘type=
‘audio/mpeg’ />
</
audio>
Baada
ya kufanya hayo basi fuata maelekezo haya, kwenye link yako uliyoikopy angalia
maneno yafuatayo kisha uyafute baada ya AUDIO ID
Link
utaikuta hivi kwa mfano
https://drive.google.com/file/d/AUDIOID/preview?/usp=shareing’ type= “audio/mpeg’
chakufanya
ni hiki maneno yaliyokolezwa kwa rangi ya kijani yafute yote na yaliyokolezwa
kwa rangi ya njano basi uyatoe na uweke maneno haya hapa chini
then
replace hayo maneno
file/d
kisha weka maneno yafuatayo
uc?export=download&id=
haya unatakiwa kuyaweka mdala wa hayo yaliyo na rangi ya njano ambapo itakuwa
https://drive.google.com/
uc?export=download&id=AUDIOID’ type= “audio/mpeg’
kwahiyo HTML itakuwa hivi
Copy
na upaste kwenye account yako kisha fanya editing ya hapo palipoandikwa Audio
Id na uweke audio id husika ya audio unayotaka kupost
< audio controls>
< source src= ‘https://drive.google.com/
uc?export=download&id=AUDIOID’ type= “audio/mpeg’ />
</ audio>
Waoo
kazi nzuri, sasa umefanikiwa kuweka audio file kwenye blogger website yako,
sasa mtu yeyote ataweza kudownload, kusikiliza na hata kucomment kwa namna
utakavyomruhusu wewe afanye, all done.
Unaswali lolote, dodosha comment kwenye
sehemu ya comment au youtube acha comment na utajibiwa kwa wakati.
Nafuraha kwamba umefanikiwa kufanya hili moja
basi darasa letu linaendelea kwa page inayofuata.
Karibu ujifunze namna gani ya kuweka video
files na videos kutoka youtube.
Ahsante
kwa kutufuatilia. Basi subscribe youtube channel yetu ya TECHNO ONLINE RICHES
na ufurahie vipindi tofauti tofauti kuhusu TECHNOLOGY AND INTERNET.
nakutakia
majukumu mema
Kwaheri na Endelea kuwa mbunifu.
By
Thobias Cosmas
Napata vitu hapa ahsante sana
ReplyDelete