JINSI YA KULINDA
DOCUMENT YAKO.
Watu wengi
huwa tunahifadhi vitu vingi kwenye mfumo wa PDF lakini bado kila mtu akiigusa
tu document yako anajua nini ulichokiweka.
Usiogope ni rahisi sana tena Zaidi ya sana na unaweza kulifanya hili kupitia kompyuta yako au kifaa chochote amabacho kinasupport PDF readers zenye uwezesho wa Ulinzi (protection)
PDF READERS NZURI KWA KAZI HII
Kuna PDF
readers nyingi sana ambazo zipo na watu wengi wanazitumia PDF reader hizo ili
kufungua na kuzisoma Pdf file ambazo wanazo. Sasa kwa hapa nakufundisha kuhusu
aina mbili za PDF readers ambazo ndizo mara nyingi huwa nazitumia na zinafanya
kazi kubwa hata ya kuedit PDF, ni maajabu lakini ujue pia PDF inaweza kueditiwa
vizuri na ukaiongezea kitu au ukapunguza kitu, kwahiyo tunaenda kujifunza tu
namna gani ya kuweka PIN/PASSWORD kwenye document yako.
PDF reader hizo ni
i.
PDF
ETRA
ii.
ADOBE
READER
Hizi ndizo
Pdf reader ambazo nazozitumia na zinafanya vizuri sana hususani katika kufungua
PDF na kuedit pia PDF hususani PDF EXTRA ndio Bora Zaidi ukilinganisha na ADOBE
READER.
Pasipokuchelewa
twende moja kwa moja kuona hatua ambazo unatakiwa kuzifuata ili uweke ulinzi
kwenye PDF yako
HATUA ZA KUFUATA KUWEKA PIN/PASSWORD KWENYE
PDF YAKO.
1. Hakikisha una PDF EXTRA na umeinstall
kwenye Computer yako.
Hujui ni mahali gani pa kuipata program hii, usiogope utabonyeza link ili
kuidownload na ukainstal kwenye PC au komputa yakp.
2. Hakikisha document yako ipo kwenye
PDF
ili uweze kuiweka kwenye mfumo wa kulindwa, kama huwezi kuweka Documents
kwenye mfumo wa pdf basi endelea kuwepo name nitakufundisha namna gani ya
kufanya ili uweke kwenye mfumo wa PDF au fuatilia video zetu youtube https://youtube.com/@technoonlineriches
3. Ifungue Pdf file yako kwa kutumia PDF
EXTRA kisha fuata hatua hizi zinazofuata
5. Bonyeza palipoandikwa PROTECT
DOCUMENT
6. Baada kubonyeza hapo utaletewa ujumbe
unaosema “changing the password requires the file to be saved. You will not be
able to undo/redo after this operation” na ikiwa imeambatana na chaguo mbili,
basi wewe bonyeza OK
7. Itafunguka kuraza ya USER RIGHTS hapo
basi utatakiwa ujaze kwa mfumo unaoutaka.
Chaguo zipo katika sehemu 3 ambazo ni
i. OPEN SOCUMENT
ii. PERMISION
iii.
ENCRYPTION
I.
OPEN DOCUMENT
Sehemu hii ni ya kwanza kabisa ambayo yenyewe inahusiana na swala la kufungua tu document, maana yake ni kwamba, ukiweka password kwenye sehemu hii basi hakuna mtu atakayeweza kufungua document hii hadi aijue password ya kufunguliA
ILI KUPATUMIA
·
Utaweka
alama ya Tick kwenye box
·
Utaweka
password yako
·
Utairudia
password yako
· Kisha bonyeza OK hapa utabonyeza ok kama nia yako nikuishia hapo ila kama unataka kwenda Zaidi basi utaenda kwa hatua ya pi.
II.
PERMISSION
Mahali hapa unaenda
kubase na vitu unavyotaka kuviruhusu au kutokuviruhusu kwenye document yako
mfano kueditiwa, kuprintiwa au kufanyiwa kitu chochote, na hapa unaweza kuweka
password yoyote kama ukiamua kutumia uliyoitumia kwenye kufungua au ukaunda
mpya tofauti na ile uliyoiweka mwanzo.
JINSI YA KUWEKA ULINZI MAHALI HAPA
·
Weka
password alafu irudie tena kwenye sehemu ya chini yake
·
Kisha
bonyeza neon OK hapo tayari utakuwa umeiaset, kwan hakuna atakaye kopi wala
kuprint document yako bila password.
ZINGATIA
Baada ya
kuweka ulinzi kwenye document yako jambo la kuzingatia ni kwamba hautakiwi
kusahau password uliyoitumia kwenye document yako, ukishaisahau basi hauna
nafasi ya kuipata tena hiyo document yako.
Kwanini?
Kwasababu hakuna chaguo la kurecover
password yako, kwahiyo hakikisha unaweka password ambayo utaikumbuka au
hakikisha unaiandika mahali ili kutunza kumbukumbu ya password yako.
Ni furaha
yangu kwamba nimeeleweka vizuri na utafanya vizuri katika kuendelea kutunza
mali zako, document zako mbali mbali. Uzuri wa hii ni kwamba hakuna mtu
atakayeweza kuitumia isipokuwa umempatia password yako.
Kulinda taarifa na mali zako ni wajibu wako.
Na hii ni mbinu ya kuzitunza mali zako.
Ahsante na
majukumu mema
By
Thobias Cosmas (Caza Von Th)
0 comments:
Post a Comment