HATUA ZA KUELEKEA MAFANIKIO YAKO

 

HATUA ZA KUELEKEA MAFANIKIO YAKO





Mafanikio

                Mafanikio ni utimilifu wa malengo yako.

Tunaposema kwamba mtu huyu amefanikiwa tunamaanisha kwamba mtu huyu amefikia malengo yake na yari yupo kwenye hatua kubwa ya yale aliyoyafanya. Hatuwezi kusema umefanikiwa na wala huwezi kusema kwamba umefanikiwa kama ulikuwa huna jambo unalolipambania, kwahiyo mafanikio yanakuja baada ya kipindi Fulani cha kulipambania jambo Fulani hadi kulitimiza.

Mafanikio yana Nyanja nyingi lakini hapa tutajifunza Zaidi kuhusu mafanikio ya kiuchumi ambayo ndio ambayo yamekuwa changamoto kwa vijana wengi na hatimae wengine kushindwa hata kuishi na kuamua kujiua kwasababu ya umasikini (failure).

Mafanikio kiuchumi maana yeke ni hatua ambayo mtu ameipiga kutoka kwenye hali ya chini ya kiuchumi hadi hali Fulani kubwa ukilinganisha na hali aliyokuwa nayo mwanzo, ambapo hapa tunasema ni ECONOMIC DEVELOPMENT, kwahiyo tunajifunza namna ya kupata maendeleo ya kiuchumi.

Baada ya kujua kwa ufupi habari hizo za maendeleo basi tutazame kwa kifupi Masikini ni nani.

Masikini ni mtu yeyote asiye na uwezo wa kukidhi mahitaji yake yaani, chakula, malazi na makazi, mtu huyu ni masikini, na mtu kuitwa tajiri maana yake anuwezo wa kupata mahitaji yake yote.

Huwezi kupata chakula kama hauna pesa, huwezi kupata mavazi mazuri kama hauna pesa, huwezi kupata matibabu mazuri kama hauna pesa, kwahiyo umasikini na utajiri vyote ni vyeo vitokanavyo na pesa.

Kuitwa masikini sio sifa nzuri kwani baadhi ya watu hujivunia na kusema yeye ni masikini jeuri, kuwa masikini sio na sio na sio sifa.

Kuna baadhi ya watu wenye Imani Fulani za kukalili kwamba Nivigumu tajiri kuingia ufalme wa mbinguni kama ngamia kupenya kwenye tundu la sindano, Jamani huu msemo usiwachukue muda, utakufa masikini na ujinga wako. Kama unasema wewe unamtumikia Mungu mtumikie huku una hela inaongeza heshima.

Basi sasa twende sambamba kujua Hatua zilizopo kuelekea mafanikio yako.

FUNGUO  ZA MAFANIKIO (Keys of success)

Basi zifuatazo ni hatua ambazo unatakiwa kuzipitia ili uweze kufanikiwa

1.       TAMBUA DHUMUNI LAKO (understanding your goals)

Katika swala la mafanikio kwa mtu anayeanza kupambana lazima ajue dhumuni lake ni nini, na kama anapambana pasipokujua nini anachopambania basi itakua ngumu sana mtu huyo kufikia mafanikio yako. Kama umepanga kufanikiwa basi Jua hicho unakiendea ni kitu gani na kina misingi ipi. Mafanikio yapo kwa kila mtu na kila mtu anaweza kufanikiwa, kama tulivyojifunza huko mwanzo kwamba mafanikio ni kufikia malengo basi hauwezi kufanikiwa kama huna malengo. Kwahiyo tambua malengo yako ni yapi ili uweze kufanikiwa. Tambua kwa kina malengo yako nah ii itakusaidia sana kufikia malengo yako. Tambua Lengo/ malengo yako kisha fuata hatua inayofuata.

2.       KUPANGILIA MALENGO YAKO NADIFU (set your smart goals)

Kupangilia malengo yako ni kitu cha msingi sana na malengo yanatakiwa kuwa nadhifu kama tulivyojifunza hapo juu, kuwa malengo ni lazima yawe nadhifu ambayo yanaweza kufanyika katika uweledi na ubora wa hali ya juu. Malengo ndio msingi mama wa mafanikio, malengo yasipokuwa vizuri hakuna mafanikio, yaani kama msingi usipokuwa imara basi hakuna nyumba inayoweza kusimama, kwahiyo malengo yanatakiwa kuwa imara ili basi mafanikio yapatikane kwa mwendokasi wa 10G kwenye internet.

Hakikisha unapangilia vizuri kuhusu malengo. kujifunza Zaidi kuhusu malengo bonyeza hapa

 

3.       ZALISHA NJIA (Generate your path)

Ukishamaliza kuweka malengo yako safi kabisa kwa kufuata hatua zote zinazostahiki katika kuandaa malengo yaani una smart goels, basi kinachofuata ni kuweka au kuzalisha njia ambazo utazitumia kufikia malengo yako. Ninapozungumzia njia ninamaanisha kuwa zalisha mbinu na namna ya kupata pesa ambayo itakufanikisha malengo yako, kwasababu naamini malengo yote yanatimizwa kwa pesa, kwahiyo lazima pesa ipatikane ili malengo yatimie.

Hakikisha unakua makini sana katika hii hatua, maana unaweza ukapanga njia ambazo mwenyewe huwezi kuzipita, lakini kumbuka kuwa lengo likiwa LINAFIKIKA basin a njia zitakuwa ZINAPITIKA.

Na katika malengo zingatia sana vyanzo vya kipato chako na ndipo utakapo weza kutimiza malengo yako. Kwahiyo zalisha njia nzuri mfano Biashara na Huduma zingine ili kufikia malengo.

 

4.       KUSHINDA MADHAIFU YAKO (overcome your weakness)

Hapa ni mahali pagumu sana lakini ni hatua ambayo ukiivuka unaweza ukafanikiwa sana. Kila mwanadamu anayomadhaifu yake, na hayo madhaifu yanamchango mkubwa sana kuelekea kile anachokifanya, na mchango wake unaweza kuwa na matokeo hasi au chanya.

Kwa Mfano, mimi ninayeandika hapa nimtu ambaye nina huruma sana, huwa sipendi nimuone mtu akiteseka wakati huo nina uwezo wa kumsaidia, na najikuta natoa msaada kwa kitu ambacho hata name nakihitaji, mwisho wa siku nabaki pasipo kufanya nilichotakiwa kufanya kwasababu ya moyo wa huruma. Kumbuka sio kwamba ni dhambi kufanya jambo hili, la hasha isipokuwa linawezekana likawa chanzo cha kunichelewesha kwenye mafanikio yangu.

Naomba hapa msomaji wangu unielewe vizuri, udhaifu ulionao unaweza ukawa kikwazo sana kuelekea mafanikio yako, udhaifu wako binafsi unaweza ukawakwazo na hili laweza kuwa sababu ya biashara nyingi sana kufungwa.

Mfano: Mtu anayependa ngono atatumia mali kuhonga

                Mtu anayependa pombe atatumia pesa kulewa

                Mtu anyependa kusaidia atatumia pesa kutoa misaada

                Mtu anayependa starehe atatumia pesa kwenye starehe

Hapa nadhani naeleweka, sina maana ya udhaifu wa magonjwa la hasha nazungumzia udhaifu wa tabia, umesikia watu wakisema ili utajirike lazima uwe BAHILI. Ni kweli punguza kutoa ili ufikie malengo yako. Kiasi kikubwa cha pesa kiwe kinachoingia na sio kinachotoka.

 

5.       JENGA NGOME YAKO (Build your fort)

Ninafuraha na hatua hii kubwa nay a msingi sana, unapozungumzia ngome unazungumzia mamlaka, ninaposema kujenga ngome yako namaanisha ngome ya mafanikio yako. Yaani tengeneza mipaka ambayo itakulimiti namna ya kutumia pesa, jiwekee sharia ambazo zitakuhukumu mwenyewe lengo tu ni kwamba ufikie malengo yako. Ngome yako sharia zako na hapo utalinda malengo yako. Badili mfumo wa maisha uliyoyaishi kabla ya kujiwekea malengo alafu jenga ngome ambayo itachagua aina ya watu wa kuingia na aina ya watu wakukuzunguka.

Unajua tuliowengi pia tunaathiriwa na watu waliotuzunguka, kwahiyo weka mipaka kwa na chagua aina ya watu wa kutembea naoi li tu ufikie malengo yako, kinyume na hapo utabaki kusema nilikuwa na malengo, nilikuwa na ndoto.

Mtu anayewaza mafanikio, huyo mzunguke kwa ngome yako,aliye kinyume achana naye haendani na sharia zako, shika amri moja, hatua mbele hakuna kuangalia nyuma, aliye nje ya ngome, kilicho nje ya ngome achana nacho jail yaliyo ngomeni kwako.

Jiamini na amini unachokitafuta utakipata.

 

6.       IISHI DUNIA YA USHAWISHI WAKO (Live the world of your psychological influence)

Inawezekana ikawa ngumu kuelewa dhima ya hatua hii lakini ni kwamba kila kitu duniani kina watu ambao wamekifanya na wakafanikiwa, na hao watu waliokifanya wakafanikiwa ni watu ambao wanaweza kukutia moyo katika safari yako na ukafanikiwa. Watu hao ndio wanaokujenga kisaikolojia na kukuandaa kifikra na kukupa mbinu mbali mbali kuelekea mpango wako, kwahiyo ukiishi katika dunia ya watu wanaofanana na wewe basi kuna nafasi kubwa na wewe kufika Zaidi kwa usalama na pasipo nguvu kubwa kama kutembea katika dunia ya watu waliokinyume na kile unachokifanya.

Kumbuka hatua ya mafanikio ni jambo linalojengeka kisaikolojia, kuna watu unaweza kukaa nao na wakakutoa kabisa kwenye mstali (Psychological blockers), kwahiyo watu kama hao sio wa kuwaweka karibu katika nyakati za kuitafuta nafasi ya mafanikio isipokuwa pambana na sikiliza waliofanikiwa kupitia hapo unapopatazamia.

Kila mtu aliumbwa kufanikiwa, Mungu hakumuumba mtu ili awe masikini, la hasha ukipambana na ukatembea vizuri basi utafanikiwa pasipo taabu yoyote

 

HATUA ZA MSINGI KUELEKEA MAFANIKIO

 

Baada ya kujua funguo za mafanikio basi hatua za mafanikio ziko tano tu

1.       Kupanga (Goals)

Weka mipango yako sawa hakikisha unamipango itakayo kuongoza

 

2.       Kujituma (workhard)

Fanya kazi kwa bidi kuiendea mipango yako kwa kutumia kidogo ulichonacho kukitafuta kikubwa

 

3.       Kujitoa na kujisimamia (commitment and consistency)

Usikubali kuyumbishwa na mtu yeyote na jitoe kwa hali na mali, mvua jua hadi ufikie malengo yako, usichoke na wala usikate tamaa, kwa shibe na njaa Jitoe kwa ajili ya ndoto zako

 

4.       Kutunza pesa (saving)

Kidogo utakachokipata kiheshimu na ukitunze kwa nidhamu na hicho kitakapokusanywa katika udogo wake kitakuwa kingi baadae (haba na haba hujaza kibaba)

 

5.       Kumuomba Mungu (praying)

Mungu ndie mbariki na mtoa ridhiki, kwahiyo kumuomba ni muhimu katika Imani yoyote ile, ili uzidi kuwa na afya na guvu tele na akufanikishe kupitia ndoto yako. Ombea sana ndoto yako Mungu hatokuacha. (Mungu hamtupi mja wake)

SUCCESS LIFE 

 

HITIMISHO

Kila penye nia pana njia, ukiweka nia ya dhati kufanikiwa lazima utafanikiwa ila usipokuwa na nia ya dhati kamwe hauwezi kufanikiwa kwani siku zote mafanikio ya mtu yanaanzia ndani yake.

Amua kufanikiwa, Amini kufanikiwa, usiogope kufanikiwa, waza kufanikiwa na pambania kufanikiwa.

Zingatia fomula ya mafanikio ni

      Plan + workhard + commitment & consistency + saving + prayers = SUCCESS

 

Ahsante sana kwa kuendelea kujifunza kupitia blog yetu, kama unaswali lolote basi uliza kwenye comment hapo chini nasi tutakujibu kwa wakati. Ahsante

 Imechapishwa na

                Thobias Cosmas Au Caza Von Th.

About TECHNO ONLINE RICHES

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

1 comments: