HATUA ZA KUELEKEA MAFANIKIO YAKO
Mafanikio
Mafanikio
ni utimilifu wa malengo yako.
Tunaposema kwamba mtu huyu amefanikiwa tunamaanisha kwamba
mtu huyu amefikia malengo yake na yari yupo kwenye hatua kubwa ya yale
aliyoyafanya. Hatuwezi kusema umefanikiwa na wala huwezi kusema kwamba
umefanikiwa kama ulikuwa huna jambo unalolipambania, kwahiyo mafanikio yanakuja
baada ya kipindi Fulani cha kulipambania jambo Fulani hadi kulitimiza.
Mafanikio yana Nyanja nyingi lakini hapa tutajifunza Zaidi
kuhusu mafanikio ya kiuchumi ambayo ndio ambayo yamekuwa changamoto kwa vijana
wengi na hatimae wengine kushindwa hata kuishi na kuamua kujiua kwasababu ya
umasikini (failure).
Mafanikio kiuchumi maana yeke ni hatua ambayo mtu ameipiga
kutoka kwenye hali ya chini ya kiuchumi hadi hali Fulani kubwa ukilinganisha na
hali aliyokuwa nayo mwanzo, ambapo hapa tunasema ni ECONOMIC DEVELOPMENT,
kwahiyo tunajifunza namna ya kupata maendeleo ya kiuchumi.
Baada ya kujua kwa ufupi habari hizo za maendeleo basi
tutazame kwa kifupi Masikini ni nani.
Masikini ni mtu yeyote asiye na uwezo wa kukidhi mahitaji
yake yaani, chakula, malazi na makazi, mtu huyu ni masikini, na mtu kuitwa
tajiri maana yake anuwezo wa kupata mahitaji yake yote.
Huwezi kupata chakula kama hauna pesa, huwezi kupata mavazi
mazuri kama hauna pesa, huwezi kupata matibabu mazuri kama hauna pesa, kwahiyo
umasikini na utajiri vyote ni vyeo vitokanavyo na pesa.
Kuitwa masikini sio sifa nzuri kwani baadhi ya watu
hujivunia na kusema yeye ni masikini jeuri, kuwa masikini sio na sio na sio
sifa.
Kuna baadhi ya watu wenye Imani Fulani za kukalili kwamba
Nivigumu tajiri kuingia ufalme wa mbinguni kama ngamia kupenya kwenye tundu la
sindano, Jamani huu msemo usiwachukue muda, utakufa masikini na ujinga wako.
Kama unasema wewe unamtumikia Mungu mtumikie huku una hela inaongeza heshima.
Basi sasa twende sambamba kujua Hatua zilizopo kuelekea
mafanikio yako.
FUNGUO ZA MAFANIKIO (Keys of
success)
Basi zifuatazo ni hatua ambazo unatakiwa kuzipitia ili uweze
kufanikiwa
1. TAMBUA DHUMUNI LAKO (understanding your
goals)
Katika swala la
mafanikio kwa mtu anayeanza kupambana lazima ajue dhumuni lake ni nini, na kama
anapambana pasipokujua nini anachopambania basi itakua ngumu sana mtu huyo
kufikia mafanikio yako. Kama umepanga kufanikiwa basi Jua hicho unakiendea ni
kitu gani na kina misingi ipi. Mafanikio yapo kwa kila mtu na kila mtu anaweza
kufanikiwa, kama tulivyojifunza huko mwanzo kwamba mafanikio ni kufikia malengo
basi hauwezi kufanikiwa kama huna malengo. Kwahiyo tambua malengo yako ni yapi
ili uweze kufanikiwa. Tambua kwa kina malengo yako nah ii itakusaidia sana
kufikia malengo yako. Tambua Lengo/ malengo yako kisha fuata hatua inayofuata.
2. KUPANGILIA MALENGO YAKO NADIFU (set your
smart goals)
Kupangilia
malengo yako ni kitu cha msingi sana na malengo yanatakiwa kuwa nadhifu kama
tulivyojifunza hapo juu, kuwa malengo ni lazima yawe nadhifu ambayo yanaweza
kufanyika katika uweledi na ubora wa hali ya juu. Malengo ndio msingi mama wa
mafanikio, malengo yasipokuwa vizuri hakuna mafanikio, yaani kama msingi
usipokuwa imara basi hakuna nyumba inayoweza kusimama, kwahiyo malengo
yanatakiwa kuwa imara ili basi mafanikio yapatikane kwa mwendokasi wa 10G
kwenye internet.
Hakikisha unapangilia vizuri kuhusu
malengo. kujifunza
Zaidi kuhusu malengo bonyeza hapa
3. ZALISHA NJIA (Generate your path)
Ukishamaliza
kuweka malengo yako safi kabisa kwa kufuata hatua zote zinazostahiki katika
kuandaa malengo yaani una smart goels, basi kinachofuata ni kuweka au kuzalisha
njia ambazo utazitumia kufikia malengo yako. Ninapozungumzia njia ninamaanisha
kuwa zalisha mbinu na namna ya kupata pesa ambayo itakufanikisha malengo yako,
kwasababu naamini malengo yote yanatimizwa kwa pesa, kwahiyo lazima pesa
ipatikane ili malengo yatimie.
Hakikisha unakua makini sana katika hii
hatua, maana unaweza ukapanga njia ambazo mwenyewe huwezi kuzipita, lakini
kumbuka kuwa lengo likiwa LINAFIKIKA basin a njia zitakuwa ZINAPITIKA.
Na katika malengo zingatia sana vyanzo vya
kipato chako na ndipo utakapo weza kutimiza malengo yako. Kwahiyo zalisha njia
nzuri mfano Biashara na Huduma zingine ili kufikia malengo.
4. KUSHINDA MADHAIFU YAKO (overcome your
weakness)
Hapa ni mahali
pagumu sana lakini ni hatua ambayo ukiivuka unaweza ukafanikiwa sana. Kila
mwanadamu anayomadhaifu yake, na hayo madhaifu yanamchango mkubwa sana kuelekea
kile anachokifanya, na mchango wake unaweza kuwa na matokeo hasi au chanya.
Kwa Mfano, mimi
ninayeandika hapa nimtu ambaye nina huruma sana, huwa sipendi nimuone mtu
akiteseka wakati huo nina uwezo wa kumsaidia, na najikuta natoa msaada kwa kitu
ambacho hata name nakihitaji, mwisho wa siku nabaki pasipo kufanya
nilichotakiwa kufanya kwasababu ya moyo wa huruma. Kumbuka sio kwamba ni dhambi
kufanya jambo hili, la hasha isipokuwa linawezekana likawa chanzo cha
kunichelewesha kwenye mafanikio yangu.
Naomba hapa msomaji wangu unielewe vizuri,
udhaifu ulionao unaweza ukawa kikwazo sana kuelekea mafanikio yako, udhaifu
wako binafsi unaweza ukawakwazo na hili laweza kuwa sababu ya biashara nyingi
sana kufungwa.
Mfano: Mtu anayependa ngono atatumia mali
kuhonga
Mtu
anayependa pombe atatumia pesa kulewa
Mtu
anyependa kusaidia atatumia pesa kutoa misaada
Mtu
anayependa starehe atatumia pesa kwenye starehe
Hapa nadhani naeleweka, sina maana ya
udhaifu wa magonjwa la hasha nazungumzia udhaifu wa tabia, umesikia watu
wakisema ili utajirike lazima uwe BAHILI. Ni kweli punguza kutoa ili ufikie
malengo yako. Kiasi kikubwa cha pesa kiwe kinachoingia na sio kinachotoka.
5. JENGA NGOME YAKO (Build your fort)
Ninafuraha na
hatua hii kubwa nay a msingi sana, unapozungumzia ngome unazungumzia mamlaka,
ninaposema kujenga ngome yako namaanisha ngome ya mafanikio yako. Yaani
tengeneza mipaka ambayo itakulimiti namna ya kutumia pesa, jiwekee sharia
ambazo zitakuhukumu mwenyewe lengo tu ni kwamba ufikie malengo yako. Ngome yako
sharia zako na hapo utalinda malengo yako. Badili mfumo wa maisha uliyoyaishi
kabla ya kujiwekea malengo alafu jenga ngome ambayo itachagua aina ya watu wa
kuingia na aina ya watu wakukuzunguka.
Unajua
tuliowengi pia tunaathiriwa na watu waliotuzunguka, kwahiyo weka mipaka kwa na
chagua aina ya watu wa kutembea naoi li tu ufikie malengo yako, kinyume na hapo
utabaki kusema nilikuwa na malengo, nilikuwa na ndoto.
Mtu anayewaza
mafanikio, huyo mzunguke kwa ngome yako,aliye kinyume achana naye haendani na
sharia zako, shika amri moja, hatua mbele hakuna kuangalia nyuma, aliye nje ya
ngome, kilicho nje ya ngome achana nacho jail yaliyo ngomeni kwako.
Jiamini na amini
unachokitafuta utakipata.
6. IISHI DUNIA YA USHAWISHI WAKO (Live the
world of your psychological influence)
Inawezekana
ikawa ngumu kuelewa dhima ya hatua hii lakini ni kwamba kila kitu duniani kina
watu ambao wamekifanya na wakafanikiwa, na hao watu waliokifanya wakafanikiwa
ni watu ambao wanaweza kukutia moyo katika safari yako na ukafanikiwa. Watu hao
ndio wanaokujenga kisaikolojia na kukuandaa kifikra na kukupa mbinu mbali mbali
kuelekea mpango wako, kwahiyo ukiishi katika dunia ya watu wanaofanana na wewe
basi kuna nafasi kubwa na wewe kufika Zaidi kwa usalama na pasipo nguvu kubwa
kama kutembea katika dunia ya watu waliokinyume na kile unachokifanya.
Kumbuka hatua ya
mafanikio ni jambo linalojengeka kisaikolojia, kuna watu unaweza kukaa nao na
wakakutoa kabisa kwenye mstali (Psychological blockers), kwahiyo watu kama hao
sio wa kuwaweka karibu katika nyakati za kuitafuta nafasi ya mafanikio
isipokuwa pambana na sikiliza waliofanikiwa kupitia hapo unapopatazamia.
Kila mtu
aliumbwa kufanikiwa, Mungu hakumuumba mtu ili awe masikini, la hasha ukipambana
na ukatembea vizuri basi utafanikiwa pasipo taabu yoyote
HATUA
ZA MSINGI KUELEKEA MAFANIKIO
Baada ya kujua funguo za mafanikio basi
hatua za mafanikio ziko tano tu
1. Kupanga (Goals)
Weka mipango yako sawa hakikisha unamipango itakayo kuongoza
2. Kujituma (workhard)
Fanya kazi kwa bidi kuiendea mipango yako kwa kutumia kidogo ulichonacho
kukitafuta kikubwa
3. Kujitoa na kujisimamia (commitment and
consistency)
Usikubali kuyumbishwa na mtu yeyote na jitoe kwa hali na mali, mvua jua
hadi ufikie malengo yako, usichoke na wala usikate tamaa, kwa shibe na njaa
Jitoe kwa ajili ya ndoto zako
4. Kutunza pesa (saving)
Kidogo utakachokipata kiheshimu na ukitunze kwa nidhamu na hicho
kitakapokusanywa katika udogo wake kitakuwa kingi baadae (haba na haba hujaza
kibaba)
5. Kumuomba Mungu (praying)
Mungu ndie mbariki na mtoa ridhiki, kwahiyo kumuomba ni muhimu katika
Imani yoyote ile, ili uzidi kuwa na afya na guvu tele na akufanikishe kupitia
ndoto yako. Ombea sana ndoto yako Mungu hatokuacha. (Mungu hamtupi mja wake)
![]() |
SUCCESS LIFE |
HITIMISHO
Kila penye nia pana njia, ukiweka nia ya
dhati kufanikiwa lazima utafanikiwa ila usipokuwa na nia ya dhati kamwe hauwezi
kufanikiwa kwani siku zote mafanikio ya mtu yanaanzia ndani yake.
Amua kufanikiwa, Amini kufanikiwa, usiogope
kufanikiwa, waza kufanikiwa na pambania kufanikiwa.
Zingatia fomula ya mafanikio ni
Plan + workhard + commitment &
consistency + saving + prayers = SUCCESS
Ahsante sana kwa kuendelea kujifunza
kupitia blog yetu, kama unaswali lolote basi uliza kwenye comment hapo chini
nasi tutakujibu kwa wakati. Ahsante
Imechapishwa na
Thobias Cosmas Au Caza Von Th.
Kumbe ndo hivi, asante sana.
ReplyDelete