KWANINI MASIKINI
HUCHELEWA KUFIKIA UTAJIRI?
Bado kunachangamoto kubwa kwa masikini kuuendea utajiri, na
mara zote masikini huwa anachelewa sana kuuendea utajiri. Na hii inatokana na
sababu mbali mbali.
MASIKINI NI NANI?
Masikini ni mtu yeyote yule asiye na maendeleo ya kiuchumi
yaani hawezi kukidhi mahitaji yake yote kama chakula, malazi na Makazi pia.
Masikini wengi hawawezi kufikia mafanikio yao kiurahisi
kwasababu ya changamoto nyingi ambazo wanazozipitia kuelekea mafanikio. Kuna
msemo unaosema “MWENYE VINGI HUONGEZEWA” msemo huu unauelewa vipi? Msemo huu
una maana kubwa sana kimsingi, maana yake kwamba mtu ambaye anacho kitu basi
anaweza kuongezewa ili afanye bora Zaidi ila mtu asiye na kitu basi hakuna haja
ya kumpatia chochote ila tu atanyang’anywa na kidogo alicho nacho.
NI MCHAKATO wa muda mrefu masikini kuufikia utajiri, ila ni
mchakato wa muda mfupi sana tajiri kuufikia umasikini endapo akishindwa kuwa na
akili ya kutunza utajiri alionao,
Unadhani ni kwanini masikini wengi huwa ni vigumu kuufikia
utajiri.
SABABU ZA MASIKINI
WENGI KUCHELEWA KUFIKIA UTAJIRI
Zifuatazo ni sababu kuu zinazosababisha masikini wengi
kuchelewa kuwa matajiri.
1. 1. Kukosa msaada wa kifedha kwenye ndoto zao
(Lack of financial support)
2. 2. Kukosa watu sahihi katika njia za mafanikio
yao (lack right people in their plan)
3. 3. Kukosa Imani ya mafanikio (give up on their
goals)
4. 4. Kuridhika na hali zao (satisfaction)
5. 5. Kukosa elimu ya uwekezaji na kujitegemea
(lack of education of investment and self-reliance)
6. 6. Mizigo mingi ya tegemezi (large number of
dependants)
1. 1. Kukosa msaada wa kifedha kwenye ndoto
zao (Lack of financial support)
Furaha yangu ni kueleweka juu ya
hili jambo, miongoni mwa watu wanaopambana sana huwa ni masikini, na lengo
kubwa nikujikwamua kutoka kwenye wimbi kubwa la umasikini. Tatizo kubwa ni
kwamba waliowengi
Ubaya Zaidi ni kwamba mtu anaweza
kuwa na ndoto Fulani na hiyo ndoto ni kubwa ambayo mtu yeyote akiifanya anaweza
akafanikiwa sana, lakini ugumu unakuja kwamba “upele umemuota asiye na kucha.”
Mara nyingi masikini huwa wanamawazo mazuri na mbinu nyingi za kibiashara
lakini ubaya unakuja sehemu moja kwamba wanashindwa kufikia zile ndoto zao
kwasababu wanakosa misaada ya kifedha kuelekea ndoto zao.
Ukosekanaji wa misaada ya kifedha
imekuwa ni sababu kubwa ya masikini kuchelewa kufikia utajiri maana muda mwingi
huutumia kutafuta pesa kwa njia zingine ili kufata malengo yake yaliyo katika
njia zingine, hii ndio sababu kubwa ya Masikini
Wengi Kuwa Na Vitu Vingi Wanavyoweza Kufanya.
2. 2. Kukosa watu sahihi katika njia za
mafanikio yao (lack right people in their plan)
Natamani kulielezea hili katika
huzunu kubwa. Siku zote ndege wafananao ndio huruka pamoja. Kwanini?, ni
kwasababu wanaongea lugha moja.
Rafiki wa masikini mkubwa huwa ni
masikini mwenzake na rafiki wa tajiri mkubwa huwa ni tajiri mwenzake, unadhani
ni kwanini? Ni kwasababu Tajiri wengi huamini kwamba masikini akiwa naye karibu
hana akili ya kumuwezesha yeye kujenga mafanikio, isipokuwa ni watu waliojaa
shida shida na kulia lia mbele zao wakitafuta msaada. Kitu kichi kinapelekea
matajiri kujitenga na masikini na hatimae masikini kuishi katika maisha ya
kimasikini na marafiki wa kimasikini.
Kwanini hili swala la kukosa watu
sahihi ni tatizo, ni kwamba, ili kupata millioni kutoka kwenye kipato cha elfu
maana yake ukutane na akili za mamilioni ambazo hizi unazipata kwa mtu mwenye
mawazo ya mamilion. Kama unataka kupiga hatu hiyo usipopata mtu mwenye akili
hiyo maana yake ni kwamba hautaweza kufikia millions utaishia elfu tu.
Watu wanaokuzunguka wakiwa sahihi
na kuendana na kile unachokiwaza inawezekana ukakifikia na ukafanikiwa.
Rafiki wa masikini ni Masikini
mwenzi hii ndio shida.
3. 3. Kukosa Imani ya mafanikio (give up on
their goals)
Mara nyingi masikini wengi hukosa
Imani ya wao kuja kuwa matajiri, kwasababu hufikia kusema “Babu alikuwa masikini, mama na baba walikuwa masikini, ndugu zangu
masikini, Nitatoboa kweli, mbona wao walishindwa?!, hapa siwezi kutoboa” mitazamo inayojengeka kwa wengi ni kwamba
kama familia au ukoo wake ni masikini basi anaamini na yeye kuwa masikini ni
kanunu za ukoo na hatimae mtu hukata tamaa na kushindwa kuendelea kupambana.
Hili ni tatizo.
Pia wengine hukata tamaa baada ya
kuona kila wanachokipanga hakina majibu kwao baada ya kukosa msaada wa kifedha
na watu sahihi kwenye safari yake ya upambanaji. Inauma sana kuongea hili
lakini lazima watu waelewe kwamba kukata tamaa kunasababisha wtu waliowengi
kuchelewa kufikia utajiri na hatimae baadhi hufa masikini. Kwanini unakata
tamaa, kwasababu umeona kizuizi usichoweza kukivuka, kwanini huwezi kukivuka,
kwasababu umeaminishwa hivyo ndani yako. Pole sana, unajichelewesha, amini kila
kitu kinawezekana.
4. 4. Kuridhika na hali zao (satisfaction)
Huwa nasikitika sana juu ya jambo
hili lakini ndilo lililopo kwa watu wengi sana, sasa twende sawa nilielezee
hili. Swala la kuridhika sio dhambi ila swala la kulidhika penye hamna hii ina
maana kwamba huelewi umeridhika na kitu gani. Utamkuta masikini anasema
“nimeridhika na hali yangu” mimi binafsi huwa nikimsikia mtu anatoa kauli hii
namuita mpumbavu asiye na akili kabisa kwasababu hakuna mtu anayeridhishwa na
kukosa mahitaji yake. Kuridhika na hali kunampelekea mtu kuwa mvivu na
kushindwa kufanya kazi za kuendelea kutafuta pesa.
Pesa ni kitu kinachotafutwa
endelevu, yaani hakuna mwisho wa kutafuta pesa labda uwe umekufa, lakini kama
upo hai basi huwezi kuridhika na pesa ulizonazo lazima uendelee kutafuta pesa
ili uwe na uhakika wa mzunguko wake. Usiridhike na Umasikini, utajikuta unahama
kwenye umasikini unaanza kuwa FUKARA. Ukiridhika kwenye umri wa miaka 15 – 50
maana yake ni kwamba miaka 60 hadi kifo utakuwa FUKARA sio masikini isipokuwa
masikini aliye bobea umasikini. Hii sio sifa, TASAF imekuja kwa niaba ya
masikini sasa kama TASAF itakutosha acha kufanya kazi.
5. 5. Kukosa elimu ya uwekezaji na kujitegemea
(lack of education of investment and self-reliance)
Baadhi ya watu wanachelewa
kufikia utajiri kwasababu ya kukosa elimu ya uwekezaji kwa kidogo walichonacho,
elimu ni swala la msingi kutolewa kwa masikini juu ya namna gani wanavyoweza
kufanya uwekezaji kwa kidogo wanachokipata. Elimu ya uwekezaji inahitajika sana
kwa masikini. Najua kuwa hata masikini awe vipi hawezi kushindwa kupata hata
elfu 50 kama ataweza kuipata hata kwa miezi 5 je, umewahi kuwaza namna gani
unaweza kuizalisha hiyo, kama hapana basi endelea kujifunza kupitia blog hii
utapata elimu kubwa sana kuelekea mafanikio yako. Jifunze kuwekeza ili uweze
kufanikiwa.
6. 6.BMizigo mingi ya tegemezi (large number
of dependents)
Hii ni tatizo kubwa ambalo
linawakumba 99% ya wapambanaji ndani ya familia za kimasikini. Shida kubwa ni
kwamba mtu huyu anyechukua muda mwingi kutafuta pesa, basi wapo watu wengi
ambao wanamtazama wote wakihitaji kupokea msaada kupitia huyo huyo mtu mmoja,
mlundikano wa mizigo mingi tegemezi kwenye familia hupelekea wengi kuishia
umasikini na hata kutikuuonja utajiri, kwasababu kila wanachokipata
kinapitiliza moja kwa moja kwenye matumizi na kuzisaidia familia.
Maisha tegemezi yanapelekea
vijana wengi kufa masikini hususani waliotokea katika familia za kimasikini.
Ili kutoboa hapa ndipo panapoleta changamoto kubwa katika mwelekeo mafanikio.
HITIMISHO
Hivi vitu vimekuwa changamoto
kubwa kuelekea utajiri kutokea umasikini, ila njia pekee ya kufanya mabadiliko
ni kujua ni mbinu gani za kufanya ili kujitoa kwenye hivyo vikwazo ili ufike
katika hatua ambayo unaweza kuifikia.
Kila mtu anaweza kuwa tajiri ila
tu chamsingi ni kujua namna gani ya kujitoa kwenye misingi ya kimasikini na
kutembea jatika misingi mipya ya utajiri.
Nifuraha yangu kuwa umeelewa, na
kama unaswali basi uliza kwenye comment box hapo chini name nitakujibu kwa
wakati, shukrani sana.
Thobias
Cosmas (caza vin Th)
0 comments:
Post a Comment