MBINU MPYA
YAGUNDULIWA YA KUTUNZA PESA
Kwa kawaida watu wengi wamekuwa wakihanagaika na kusumbuka
kwa namna gani nzuri ambayo wanaweza kuitumia ili kutunza pesa zao kuelekea
malengo makubwa waliojiwekea katika maisha yao. Kwa bahati mbaya waliowengi
hushindwa kufikia malengo yao kwasababu tu wameshindwa kujua namna gani ya
kufanya ili kuweka au kutunza pesa zao.
Mfumo wa maisha ya uchumi umekuwa mgumu sana ukilinganisha
na nyakati za zamani na mbaya Zaidi kwasasa mtu kumiliki na kutawala kitu
chochote kimekuwa ni mtihani mkubwa kwa namna kwamba kwasasa hakuna chakupewa
isipokuwa chakuhangaikia.
Kulingana na dhana hii iliyopo katika mfumo wa maisha basi
inapelekea watu wengi kutumia nguvu sana kuweka pesa ili angalau waje kufikia
hali ya kumiliki na kutawala. Ukweli halisi ni kwamba, tatizo la kutunza pesa
kwa ajili ya malengo linawakumba sana vijana ambao bado wanajitafuta na hata
watu wazima na Wazee pia na hii ni kwasababu kuweka/ kutunza pesa ni sawa na
hatua kubwa ya kujitoa sadaka. Inawezekana ikawangumu kunielewa.
Watu wengi wanajaribu mbinu mbalimbali hata kuamua
kutengeneza vitu mbalimbali vya kutunzia pesa lakini bado changamoto inakuja
pale pale kwamba pesa ile wanaihitaji kabla ya wakati wa malengo na hawana
namna nyingine lazima waiguse ili iwasaidie kwa msemo unaosema mtu na chake.
Ni kweli kwamba mtu husaidiwa na kitu chake mwenyewe, hakuna
mtu anayeweza kusaidiwa na kitu kichokuwa chakwake hivyo chako ndio msaada
wako.
Katika nakala hii naenda kuelezea mbinu mpya ya kutunza fedha
ambayo imegunduliwa na si kwamba haikuwepo ispokuwa watu wengi hawakuielewa
kwamba inawezekana ikawa msaada kwao kutunza pesa. Na kabla sijaielezea basi
naomba nijalibu kuelezea vitu baadhi ambavyo watu wamefanya ili kutunza pesa
zao na bado hatima yake zile pesa zikatumika kabla ya malengo.
VYOMBO VYA KUHIFADHIA
PESA
1. VIBUBU.
Watu wengi wamekuwa wakitumia
nguvu nyingi kutengeneza vibubu ambavyo zinawasaidia kutunza fedha zao
wakitarajia ndani ya muda Fulani basi watavunja kibubu chao na kuangalia kuna
kiasi gani cha pesa walichokikusanya. Vyema, baadhi hufanikiwa kufanya jambo
hili na kufikia malengo yao kwa namna hiyo, lakini njia hii huwa inasumbua sana
hususani kwa watu wanaopata pesa kwa ngekewa (kwa kubahatia). Hawa watu
hujikuta kutafuta mbinu za kutoa pesa kwenye vibubu vyao na hata wengine kwenda
kuvivunja na kutoa kilichomo ili kiwakomboe. OOhh! Hatari sana, licha ya nguvu
kubwa ya kutumia kibubu bado njia hii imekuwa ngumu sana katika kuweka fedha
ili uje kuzitoa baadae.
2. BANK
Benki ni mahali panapoaminika
sana kutunzia pesa, lakini changamoto kubwa ambayo inatokea ni kwamba Benki
zimerahisisha namna ya utoaji wa pesa mahali popote ulipo, na hii kitu
imepelekea watu wengi kutokufikia malengo yao na hatimae akiba zao kuisha.
Namaanisha, mfumo wa simbanking ni mfumo ambao unamrahisishia mtu kutoa pesa mahali
popote kupitia simu yake, na mtu akishajiunga na simbank anaweza kufanya
muamala na pesa anayoihitaji kumfikia mkononi mwake, hii imechangia pia kwa
wengi kushindwa kufikia malengo yao baada ya kukutana na urahisi wa kutoa pesa
zao mahali popote walipo. Kwa Benk kusitisha huduma ya simbank ni kitu
kisichowezekana kwasababu namna miamala inavyofanyika basi nao hufaidika vyivyo
hivyo pamoja na serikali, huenda hujanielewa ila namanisha unapotoa pesa
kutokea benki basi kuna % zinabaki benk, kuna % zinaingia kwenye serikali, na
kama umetumia mtandao wa simu kwa simbank nao pia unaingiza % kadhaa pindi
utakapoitoa kwao na serikali tena % kadhaa, maana yake simbank inafaida kubwa
kwa serikali kwahiyo kusitishwa kwa huduma hii ni jambo lisilowezekana.
Pia shida ya kuweka pesa bank ni
kwamba kuna makato wakati wa kuitoa pesa yako, na hapa panaweza kuathili namna
ya malengo yako ya kifedha.
3. WATU UNAO WAAMINI.
Watu wengi wamekuwa wakiwekeza
pesa kwa watu wanao waamini ambao kwa kawaida na hao watu wanamahitaji yao, hii
ni changamoto kubwa kwa wengi, unawekeza pesa na mwisho wa siku unaenda kwa
yule mtu unakuta pesa zimeshatumika, badala ya kuwa Store imekuwa consumer,
mwisho wa siku mnaingia katika hatua mpya ya kudaiana ambayo haikuwa lengo la
kuweka pesa yako.
Kingine ni kwamba unapowekeza
pesa kwa mtu, ni mwanadamu anakuelewa utakapomwambia uhitaji wako, kwahiyo
anaweza kukupatia muda wowote kwani pesa sio yake ila ni yako, hii nayo bado
imekuwa ni changamoto sana ya namna gani mtu unaweza kuhifadhi fedha.
4. VIKOBA
Kuna vyombo vingine ambavyo sasa
vinatumika kama sehemu ya kuweka pesa, vikoba ni vikundi vya watu wenye jinsia
moja au jinsia tofauti ambavyo hukenga kuhifadhi fedha na mwisho wa siku kugana
pesa zile, lakini mbaya Zaidi iliyopo katika vikoba ni kwamba kuna swala la
mikopo ndani ya vikoba, sasa hii sio kuwekeza pesa isipokuwa ni kupata sehemu
ambapo ukipata shida unaweza kupata pesa na baadae utairudisha, mbaya Zaidi
ukishindwa kulipa ni kwamba Pesa yako uliyoiweka hautaipata na kama faida
itapatikana basi inawezekana upate kidogo au usipate kabisa na hata vitu vya
ndani ulivyoweka kama dhamana vikachukuliwa na kwenda kuuzwa kwa ajili ya
kurejesha pale ulipochukua. Hii mbaya sana lakini hakuna namna wengi
wanashiriki na baadhi hufanikiwa hususani wasio na Tamaa.
5. AKAUNTI ZA SIMU
Watu wengi pia wamekuwa wakitumia
simu zao kama sehemu ya kuhifadhia pesa zao na hii pia imekuwa changamoto
kwasababu simu ni kitu ambacho muda wote kipokaribu na muhifadhi pesa, sasa
changamoto inakuja kuwa kubwa kwamba Account inafikika.
Wengine hata wakiishiwa vocha
huenda kwenye account zao na kuamua kutoa pesa inayopatikana huko na kuibadili
kuwa salio au kifurushi kwa ajili ya matumizi yake.
Uwekaji wa pesa umekuwa ni
changamoto sana na Malengo imekuwa kazi sana kuyafikia na hatimae kubaki kila
siku kama ulivyo pasipokufikia malengo uliyojiwekea. Basi kwa namna hii
tunajaribu kila siku kutengeneza mbinu mpya za namna gani ya mtu kutunza pesa kuendea
malengo yake aliyojiwekea. Basi katika nakala hii ni mbinu pendekezi ambayo
naweza kuitoa ili kwamba mtu aweze kuhifadhi pesa yake na pesa iwe salama na
aweze kuipata kwa wakati kuendea lengo lake alilojiwekea.
MBINU MPYA YA KUTUNZA PESA KUELEKEA MALENGO.
Kwa kawaida watu wengi Imani zao
zomewekwa katika serikali na baadhi ya watu na mashirika tofauti tofauti, na
Imani zao zipo kwao na wanaamini kwamba serikali itaweza kuwasaidia na
kuwafanya watu kufikia malengo yao.
Wazo ni kwamba, kwanini serikali
isiunde chombo maalumu ambacho kitashughulika na swala la watu kuweka akiba zao
na kuuza malengo yao kwao na mwisho wa siku watakapoona akiba ya yule mtu
imetimia na anaweza kutimiza malengo yake, wakamsaidia kumtimizia malengo yake
kisha maisha mengine yakaendelea?
Mfano:
Ninalengo
la kupata kiwanha Mkoani Dodoma, na hapa niliposina pesa kamili ila nikisema
nipambane mwaka mmoja naweza kupata milioni 5 ambazo hizo zaweza kunipatia
kiwanja, basi nitaenda kwenye body hiyo na nitatoa maelezo yangu na muda ambao
nitatumia ili kufikisha kiasi hicho, kisha nitaanza utekelezaji na siku hiyo
kuna kiasi nitakachoenda nacho kuhifadhi kama kianzio katika ratiba yangu,
kwahiyo nitahusika kutoa pesa hiyo mahali popote nilipo hata kwa njia ya simu
na mwisho wa siku pesa yangu ikitimia, basi chombo kile kitanitafutia kiwanja
na kunikabidhi kikiwa kimekamilika, serikali hamuoni hili kama linaweza kuwa
msaada kwa watanzania wengi.
Hili jambo linaweza kuwa msaada,
hili si kwa serikali tu hata mtu binafsi anaweza kufanya jambo hili ambaye
anaamini kwamba anaweza kuwasaidia watu kufikia malengo yao waliyojiwekea. Hili
ni jambo ambalo nimeliwaza Zaidi ya miaka mitano na leo nimeona basi nilitoe
kwa watanzania na watu wote walisikie na walitolee hoja kwa namna moja au
nyingine.
Jambo hili linawalenga sana
vijana wapambanaji na watafutaji wa kesho zao, nisiwafiche vijana kuna mahali
tunapokwama na hapo wengi hatupajui.
VIJANA TUNAKWAMA WAPI?
Vijana waliowengi kwenye mfumo wa
utafutaji wa maisha tuna mahali ambapo tuna kwama na hii sehemu ni sehemu pekee
ambayo wengi walitupiga hatua hata kidogo wanaitumia ili kutuumiza sisi na
mbaya Zaidi hatuelewi kwamba tunaumia.
Kijana ni mtu yeyote mwenye umri
miaka 18-45, japo mimi huwa napenda kusema kuwa kijana ni mtu anaye jitambua
vizuri yaani yupo kwenye nafasi ambayo anaelewa kile anachokifanya kina matokeo
gani, ambapo kiwango hiki mara nyingi kinaanza kwa watu wanye umri miaka 15 na
kuendelea, ukiangalia vizuri miaka 15 wengi wamekwisha hitimu darasa la saba
kwa sasa.
Vijana waliowengi kwa kawaida
wanajishughulisha na shughuli mbali mbali za maisha na lengo kubwa ni kuondoa
umasikini ambao upo kwao na familia zao. Kwanini nasema kwao na familia zao,
nasema kwao na familia zao kwasababu, kijana hawezi kuwa masikini kama familia
yake ni matajiri, la hasha, ila kwakuwa familia ni masikini basi hata kijana
anauvaa umasikini ule uliopo katika familia, kwahiyo vijana wanapambana kutoa
gamba la umasikini kwake na familia yake.
Kwa kawaida vijana wengi wamekuwa
wakifanya shughuli nyingi za kuajiliwa na baadhi wamejiajili na waliojiajili ni
wachache kuliko walioajiliwa katika sekta tofauti za kiserikali na za
kibinafsi.
Vijana wanakwama wapi? Kwa namna
vijana wanavyopambana tunatarajia kwamba vijana wamiliki Zaidi kuliko wale
ambao si wa pambanaji kama wao, lakini unaweza kushangaa kwamba watu wazima ni
watu wanaomiliki ukilinganisha na vijana.
Kuna mahali vijana wanapokwama na
hapo ndipo ambapo watu wazima wametupiga hatua na kutuacha nyuma (lakini sio
watu wazima wote).
Niliwahi kukutana na swali hili
kwa wazee kadhaa
Swali “mbona bijana wasasa ni wavivu na hawana hata viwanja wala nyumba?”
Ukweli nilimuangalia sana huyo
mzee na sikumpatia jibu kwa haraka, ila ilibidi nousome mtazamo yake kuelekea
hilo swali, basi nilimjibu na kumuuliza swali
Jibu: “hapana, vijana si wavivu isipokuwa wewe unawaona kuwa ni wavivu
kulingana na vitu unavyomiliki, ukweli ni kwamba vijana wanapambana sana
isipokuwa changamoto ni ugumu wa upatikanaji wa pesa na vyanzo vizuri vya
uhakika wa pesa na hii inapelekea vijana kuonekana wwavivu wasio na kazi,
kuhusu swala la viwanja, baba nilazima uzipime nyakati na uelewe nyakati pia,
miaka ya 80 viwanja mtu ulikuwa unajipimia kwasababu maeneo yalikuwa wazi
lakini kwasasa maeneo mengi yameshakaliwa na watu yamekuwa na thamani
kulinganisha na nyakati zenu, miaka yenu mtu kumiliki Hekali 10 hadi 20 ilikuwa
rahisi ila kwasasa ni ghari sana, vijana wanatafuta, usiwatazame kwa namna
unavyowatazama, alafu usilinganishe 1950 na 2024 utapata changamoto kubwa
kichwani kwako.”
Alijibu: “Ila ni kweli mwanabgu, kwasasa hali ngumu sana, poleni ila fanyeni
yote kwa akili, wekezeni, ishini kwa kuwekeza”
Huu ni ukweli usiofichika kwamba
maisha ni magumu na watu tunapambana, isipokuwa tunafeli sana katika kutumia
akili na heshima na hofu katika vyote tunavyovifanya na kuvipata pia.
Vijana
Tunafeli hapa
1. KUKOSA MAARIFA
Vijana wengi hatutumii akili
katika kufanya mambo na hii ni kwasababu vijana tuliowengi hatupendi kujifunza
isipokuwa tunapenda kujifurahisha.
Vijana wengi wa kitanzania sio wapenzi
wa kusoma vitabu vinavyoelezea mambo ya mafanikio ila niwa taalamu wakusoma
hadithi za mapenzi na post za mapenzi, badala ya kuwa busy kutafuta mambo
yanayowasaidia kupiga hatua za kiuchumi wanapiga mbio kutafuta mambo
yanayowasaidia kupiga hatua kwenye mapenzi. Sasa jambo hili linawapelekea
waliowengi kushindwa kufanya mambo ya maana na hata pesa wanazozipata zinaishia
kwenye mapenzi na mahusiano basi.
Mtu yuko radhi kununua Mkongo kwa
Elfu 50 akamkomoe binti ila hayuko radhi kutumia elfu 10 kununua kitabu cha
mbinu za mafanikio. Inachekesha lakini ndio uhalisia tulionao kwa vijana wa
Tanzania.
Mbaya Zaidi kwasababu ya mapenzi
vijana wanatoa hata pesa za mabosi zao kumpatia mwanamke (kuhonga) ili apate
hata masaa 2 ya kufanya mapenzi naye kuliko kuitumia hiyo pesa kuwaza nmana
gani nitaweza kuanzisha biashara yako.
Heshima kwenu wanachama Hai wa UWABATA
(Umoja wa wanaume Bahili Tanzania). Mapenzi imekuwa ni changamoto kubwa
inayoharibu ndoto na mpangilio wa maisha ya vijana wengi, ni upumbavu ambao umevitawala
vichwa vya vijana wengi, ni mdudu uliotawala vichwa vya vijana wengi.
Vijana hatutumii akili naam
hatutumii maarifa kwasababu hatuna hayo maarifa, na hatuna hayo maarifa
kwasababu hatuyatafuti, ili kufanikiwa lazima kutumia akili na maarifa ya nyongeza
kutoka kwa watu mbali mbali waliofanikiwa. Tafuta akili
2. KUTOKUHESHIMU
Ndugu zangu, Vijana wenzangu na
rafiki zangu pia, unajua kuheshimu ni kitu kikubwa sana, yani mtu kuwa na
heshima ni jambo ambalo linaweza kukufanya wewe kufanikiwa, heshima sio kusema
“Shikamoo….!!” Hapana ispokuwa heshima ni upendo/ nidamu ya ndani kwa mtu au
kitu chochote kwa uwezo wake, ubora wake au mafanikio yake na na kuendelea.
Kuwa ma heshima maana yake ni kuona thamani ya kile kitu na kukichukulia cha
thamani, Heshima ndio kitu pekee kinachoweza kumfanya kijana afanikiwe.
Kijana anatakiwa kuheshimu kila
mtu anayemuona, haijalishi anamfahamu au hamfahamu, kwasababu pesa zina watu na
watu wana pesa, usipo waheshimu watu maana yake huna heshima na mahali pesa
zilipo, huu ndio ukweli halisi.
Pesa inatakiwa iheshimiwe kwa
kiwango kikubwa, yaani hata ukiwa na senti 1 unasababu ya kuiheshimu pesa na
kuiona ya thamani, kwani pesa kwa kawaida ni ngumu kuipata lakini ni rahisi
sana kuitumia.
Pesa unayoipata ukiiheshimu,
lazima uitumie wa nidhamu, matumizi mazuri ya pesa yanategemeana na nidhamu
kubwa uliyonayo katika matumizi ya Pesa hiyo. Vijana wa hovyo, hawaelewi nini
Thamani ya pesa wakiwa nayo, wanaelewa thamani ya pesa wasipokuwa nayo. Huu ni
upumbavu uliokithiri.
Kwasababu ya watu wengi
kutokuheshimu pesa basi inafikia kuwasema vibaya vijana wenzao waliofanikiwa
kwa kuwapa majina kama mafrimason na kadhalika, lakini hawajui namna gani
walivyohangaika hadi kufikia hapo walipo. Vijana hawaheshimu pesa na hawaelewi
faida ya kuheshimu pesa, mwisho wa siku umasikini unawatawala. Siku zote
utakacho kiheshimu kitakuheshimu, ukiiheshimu pesa nayo pia itakuheshimu.
3. KUPOTEZA KUMBUKUMBU
Vijana tuliowengi huwa tunapoteza
kumbukumbu ya wapi tulipotokea na wapi tunapoelekea, na hii inatufanya tuwe
vijana tuliochanganyikiwa, kumbukumbu ni kitu kinachoweza kumsaidia mtu
kujielewa yeye ni nani, kutokuwa na kumbukumbu kunapoteza kabisa uhalisia wa
kijana kuishi katika ndoto yake na hatimae kuwa bendela fuata upepo, kumbukumbu
ni msingi sana kuelekea mafanikio ya aina yoyote, Kwa kadri tunavyo vaa Crazy
Jins ndivyo tunavyokuwa na Crazy Minds, ukuivaa crazy jins alafu na wewe
hujielewi hujakpsea ukosahihi kwasababu ndivyo ulivyo. Usinielewe vibaya, nina
maana hii, ukifanya kitu cha kijinga na mtu akidhani kwamba uko sahihi akasahau
kwamba haukumbuki ulikotoka na wala hujui unakokwenda atakuwa haelewi kwamba
jina la vazi linasadifu yaliyomo.
Iko hivi, kumbuka wapi ulipo na
wapi unapoelekea, ni rahisi sana wewe kufanikiwa kwenye maisha yako endapo
utakuwa angalau na kumbukumbu ya maisha yako na hatima yako wewe na familia
yako, na hapa utaheshimu kile kidogo unachokipata na utakiona kuwa cha thamani sana
Zaidi ya mambo yoyote, unaweza kumkuta mtu anakwambia maisha magumu, ukimuuliza
kwanini atakwambia pesa ngumu, ukimuulia kwani unampango gani na pesa,
utakutana na majibu ya ajabu ajabu. Vijana Hatujitambui.
4. HATUHESHIMU MUDA
Kwa kutokujua thamani ya muda
tulionao wengi wanaamini watapata kesho, na hiyo kesho inaandaliwa lini? Sijui,
huu ni ujinga ambao asilimia kubwa ya vijana tunao, na tunasema tutapata kesho
alafu hatuna kitu tunachokifanya leo kitakachotupa faida kesho, Tunasubiri
Mungu atujalie tufanikiwe, sikia rafiki, hata waliokufa masikini pia walikua
wanasali, wanafunga na wanaomba sana naam Imani haiwezi kuzaa matunda kama
anaye amini hajishughulishi, ndio maana hata maandiko yanasema “Mungu
anazibariki kazi za mikono yako” Ayubu 1:10 “kazi za mikono yake umezibarikia.
Nayo mali yake imeongezeka katika nchi” aiseee Mungu anambariki anayefanya kazi
tena sio kazi kwa mikono tu na awe na akili, usipokuwa na akili huwezi
kufanikiwa hadi unakufa. Heshimu muda ulionao, fanya mambo kwa ratiba na muda hapa
utafanikiwa kwa nafasi kubwa sana,
5. HATUNA MALENGO
Swala la kuwa na malengo ni
changamoto sana, vijana wengi tunamalengo lakini sio malengo hai, tunayomalengo
ambayo yapo tu na yatafanikiwa kwa mpango wa Mungu sio kwa jitihada zetu
kuyatimiza. Kuwa na malengo ya namna hii ni sawa tu na mtu asiye na malengo
yaani unaishi ishi tu kuendana na chochote kitakachokuja, Kijana una kila
sababu za kujiwekea malengo yako, chochote kitakachokuja nje ya malnego yako
maana yake ni kwamba sio kitu sahihi kuwepo upande wako, hivyo kipige chini
kisha endelea na mambo meninge maana hicho hakikufai kabisa. Naongeza kusema
panga malengo, weka malengo, simamisha malengo hapo utafanikiwa
6. HATUYAISHI MALENGO
Swala la kuwa na malengo na swala
la kuyaishi malengo, ni maswala mawili tofauti, unaweza kuwa na malengo lakini
usiweze kuyaishi hayo malengo, vijana tuliowengi tunafeli kwasababu tuna
malengo ambayo hatuyaishi, ukiwa na malengo hakikisha unayaishi yaani
unayafuata, yanakuongoza chakufanya ili
kuyafikia, ukishindwa kuyafuata malengo yako basi hauna maana ya kuwa na
malengo, kuyaishi malengo ni jitoa sadaka, yani kubali kuacha kila kitu na
ufanye swala linaloleta mafanikio ya malengo yako, panga kufanikiwa, alafu
yatafute mafanikio.
HITIMISHO.
Maisha ya ujanani ni maisha yenye
changamoto nyingi, lakini ni mahali pekee unapoweza kutengeneza kesho yako
iliyo nzuri na ya kuheshimiwa na kukumbukwa na watu. Wekeza muda wako katika
kufanya na kuwaza mambo yenye tija na maisha yako, mambo yasio na faida achana
nayo na utazame tu ulipo na unapoelekea. Najua ukiishi kwa kufuata ndoto zako
kufanikiwa lazima.
Unaswali lolote?
Usiogope, comment hapo chini na
nitakuja kukujibu kwa wakati
Naitwa THOBIAS COSMAS ukipenda niite Caza
von Th. Cognitiologistic
Hahahahahaaaaaa dahh nimebidi nicheke kwanza, ila umefundisha na umeelekeza vyema, bado nitakuwa na swali baadae maana huo ushauri ni kuntu
ReplyDelete