NAMNA YA KUJIWEKEA AKIBA (HOW TO SAVE

 

MBINU MPYA YAGUNDULIWA YA KUTUNZA PESA



Kwa kawaida watu wengi wamekuwa wakihanagaika na kusumbuka kwa namna gani nzuri ambayo wanaweza kuitumia ili kutunza pesa zao kuelekea malengo makubwa waliojiwekea katika maisha yao. Kwa bahati mbaya waliowengi hushindwa kufikia malengo yao kwasababu tu wameshindwa kujua namna gani ya kufanya ili kuweka au kutunza pesa zao.

Mfumo wa maisha ya uchumi umekuwa mgumu sana ukilinganisha na nyakati za zamani na mbaya Zaidi kwasasa mtu kumiliki na kutawala kitu chochote kimekuwa ni mtihani mkubwa kwa namna kwamba kwasasa hakuna chakupewa isipokuwa chakuhangaikia.

Kulingana na dhana hii iliyopo katika mfumo wa maisha basi inapelekea watu wengi kutumia nguvu sana kuweka pesa ili angalau waje kufikia hali ya kumiliki na kutawala. Ukweli halisi ni kwamba, tatizo la kutunza pesa kwa ajili ya malengo linawakumba sana vijana ambao bado wanajitafuta na hata watu wazima na Wazee pia na hii ni kwasababu kuweka/ kutunza pesa ni sawa na hatua kubwa ya kujitoa sadaka. Inawezekana ikawangumu kunielewa.

Watu wengi wanajaribu mbinu mbalimbali hata kuamua kutengeneza vitu mbalimbali vya kutunzia pesa lakini bado changamoto inakuja pale pale kwamba pesa ile wanaihitaji kabla ya wakati wa malengo na hawana namna nyingine lazima waiguse ili iwasaidie kwa msemo unaosema mtu na chake.

Ni kweli kwamba mtu husaidiwa na kitu chake mwenyewe, hakuna mtu anayeweza kusaidiwa na kitu kichokuwa chakwake hivyo chako ndio msaada wako.

Katika nakala hii naenda kuelezea mbinu mpya ya kutunza fedha ambayo imegunduliwa na si kwamba haikuwepo ispokuwa watu wengi hawakuielewa kwamba inawezekana ikawa msaada kwao kutunza pesa. Na kabla sijaielezea basi naomba nijalibu kuelezea vitu baadhi ambavyo watu wamefanya ili kutunza pesa zao na bado hatima yake zile pesa zikatumika kabla ya malengo.

VYOMBO VYA KUHIFADHIA PESA

1.       VIBUBU.

Watu wengi wamekuwa wakitumia nguvu nyingi kutengeneza vibubu ambavyo zinawasaidia kutunza fedha zao wakitarajia ndani ya muda Fulani basi watavunja kibubu chao na kuangalia kuna kiasi gani cha pesa walichokikusanya. Vyema, baadhi hufanikiwa kufanya jambo hili na kufikia malengo yao kwa namna hiyo, lakini njia hii huwa inasumbua sana hususani kwa watu wanaopata pesa kwa ngekewa (kwa kubahatia). Hawa watu hujikuta kutafuta mbinu za kutoa pesa kwenye vibubu vyao na hata wengine kwenda kuvivunja na kutoa kilichomo ili kiwakomboe. OOhh! Hatari sana, licha ya nguvu kubwa ya kutumia kibubu bado njia hii imekuwa ngumu sana katika kuweka fedha ili uje kuzitoa baadae.





2.       BANK

Benki ni mahali panapoaminika sana kutunzia pesa, lakini changamoto kubwa ambayo inatokea ni kwamba Benki zimerahisisha namna ya utoaji wa pesa mahali popote ulipo, na hii kitu imepelekea watu wengi kutokufikia malengo yao na hatimae akiba zao kuisha. Namaanisha, mfumo wa simbanking ni mfumo ambao unamrahisishia mtu kutoa pesa mahali popote kupitia simu yake, na mtu akishajiunga na simbank anaweza kufanya muamala na pesa anayoihitaji kumfikia mkononi mwake, hii imechangia pia kwa wengi kushindwa kufikia malengo yao baada ya kukutana na urahisi wa kutoa pesa zao mahali popote walipo. Kwa Benk kusitisha huduma ya simbank ni kitu kisichowezekana kwasababu namna miamala inavyofanyika basi nao hufaidika vyivyo hivyo pamoja na serikali, huenda hujanielewa ila namanisha unapotoa pesa kutokea benki basi kuna % zinabaki benk, kuna % zinaingia kwenye serikali, na kama umetumia mtandao wa simu kwa simbank nao pia unaingiza % kadhaa pindi utakapoitoa kwao na serikali tena % kadhaa, maana yake simbank inafaida kubwa kwa serikali kwahiyo kusitishwa kwa huduma hii ni jambo lisilowezekana.

Pia shida ya kuweka pesa bank ni kwamba kuna makato wakati wa kuitoa pesa yako, na hapa panaweza kuathili namna ya malengo yako ya kifedha.



3.       WATU UNAO WAAMINI.

Watu wengi wamekuwa wakiwekeza pesa kwa watu wanao waamini ambao kwa kawaida na hao watu wanamahitaji yao, hii ni changamoto kubwa kwa wengi, unawekeza pesa na mwisho wa siku unaenda kwa yule mtu unakuta pesa zimeshatumika, badala ya kuwa Store imekuwa consumer, mwisho wa siku mnaingia katika hatua mpya ya kudaiana ambayo haikuwa lengo la kuweka pesa yako.

Kingine ni kwamba unapowekeza pesa kwa mtu, ni mwanadamu anakuelewa utakapomwambia uhitaji wako, kwahiyo anaweza kukupatia muda wowote kwani pesa sio yake ila ni yako, hii nayo bado imekuwa ni changamoto sana ya namna gani mtu unaweza kuhifadhi fedha.

4.       VIKOBA

Kuna vyombo vingine ambavyo sasa vinatumika kama sehemu ya kuweka pesa, vikoba ni vikundi vya watu wenye jinsia moja au jinsia tofauti ambavyo hukenga kuhifadhi fedha na mwisho wa siku kugana pesa zile, lakini mbaya Zaidi iliyopo katika vikoba ni kwamba kuna swala la mikopo ndani ya vikoba, sasa hii sio kuwekeza pesa isipokuwa ni kupata sehemu ambapo ukipata shida unaweza kupata pesa na baadae utairudisha, mbaya Zaidi ukishindwa kulipa ni kwamba Pesa yako uliyoiweka hautaipata na kama faida itapatikana basi inawezekana upate kidogo au usipate kabisa na hata vitu vya ndani ulivyoweka kama dhamana vikachukuliwa na kwenda kuuzwa kwa ajili ya kurejesha pale ulipochukua. Hii mbaya sana lakini hakuna namna wengi wanashiriki na baadhi hufanikiwa hususani wasio na Tamaa.

5.       AKAUNTI ZA SIMU

Watu wengi pia wamekuwa wakitumia simu zao kama sehemu ya kuhifadhia pesa zao na hii pia imekuwa changamoto kwasababu simu ni kitu ambacho muda wote kipokaribu na muhifadhi pesa, sasa changamoto inakuja kuwa kubwa kwamba Account inafikika.

Wengine hata wakiishiwa vocha huenda kwenye account zao na kuamua kutoa pesa inayopatikana huko na kuibadili kuwa salio au kifurushi kwa ajili ya matumizi yake.

 

Uwekaji wa pesa umekuwa ni changamoto sana na Malengo imekuwa kazi sana kuyafikia na hatimae kubaki kila siku kama ulivyo pasipokufikia malengo uliyojiwekea. Basi kwa namna hii tunajaribu kila siku kutengeneza mbinu mpya za namna gani ya mtu kutunza pesa kuendea malengo yake aliyojiwekea. Basi katika nakala hii ni mbinu pendekezi ambayo naweza kuitoa ili kwamba mtu aweze kuhifadhi pesa yake na pesa iwe salama na aweze kuipata kwa wakati kuendea lengo lake alilojiwekea.

 

MBINU MPYA YA KUTUNZA PESA KUELEKEA MALENGO.

Kwa kawaida watu wengi Imani zao zomewekwa katika serikali na baadhi ya watu na mashirika tofauti tofauti, na Imani zao zipo kwao na wanaamini kwamba serikali itaweza kuwasaidia na kuwafanya watu kufikia malengo yao.

Wazo ni kwamba, kwanini serikali isiunde chombo maalumu ambacho kitashughulika na swala la watu kuweka akiba zao na kuuza malengo yao kwao na mwisho wa siku watakapoona akiba ya yule mtu imetimia na anaweza kutimiza malengo yake, wakamsaidia kumtimizia malengo yake kisha maisha mengine yakaendelea?

Mfano:

        Ninalengo la kupata kiwanha Mkoani Dodoma, na hapa niliposina pesa kamili ila nikisema nipambane mwaka mmoja naweza kupata milioni 5 ambazo hizo zaweza kunipatia kiwanja, basi nitaenda kwenye body hiyo na nitatoa maelezo yangu na muda ambao nitatumia ili kufikisha kiasi hicho, kisha nitaanza utekelezaji na siku hiyo kuna kiasi nitakachoenda nacho kuhifadhi kama kianzio katika ratiba yangu, kwahiyo nitahusika kutoa pesa hiyo mahali popote nilipo hata kwa njia ya simu na mwisho wa siku pesa yangu ikitimia, basi chombo kile kitanitafutia kiwanja na kunikabidhi kikiwa kimekamilika, serikali hamuoni hili kama linaweza kuwa msaada kwa watanzania wengi.

Hili jambo linaweza kuwa msaada, hili si kwa serikali tu hata mtu binafsi anaweza kufanya jambo hili ambaye anaamini kwamba anaweza kuwasaidia watu kufikia malengo yao waliyojiwekea. Hili ni jambo ambalo nimeliwaza Zaidi ya miaka mitano na leo nimeona basi nilitoe kwa watanzania na watu wote walisikie na walitolee hoja kwa namna moja au nyingine.

Jambo hili linawalenga sana vijana wapambanaji na watafutaji wa kesho zao, nisiwafiche vijana kuna mahali tunapokwama na hapo wengi hatupajui.

VIJANA TUNAKWAMA WAPI?

Vijana waliowengi kwenye mfumo wa utafutaji wa maisha tuna mahali ambapo tuna kwama na hii sehemu ni sehemu pekee ambayo wengi walitupiga hatua hata kidogo wanaitumia ili kutuumiza sisi na mbaya Zaidi hatuelewi kwamba tunaumia.

Kijana ni mtu yeyote mwenye umri miaka 18-45, japo mimi huwa napenda kusema kuwa kijana ni mtu anaye jitambua vizuri yaani yupo kwenye nafasi ambayo anaelewa kile anachokifanya kina matokeo gani, ambapo kiwango hiki mara nyingi kinaanza kwa watu wanye umri miaka 15 na kuendelea, ukiangalia vizuri miaka 15 wengi wamekwisha hitimu darasa la saba kwa sasa.

Vijana waliowengi kwa kawaida wanajishughulisha na shughuli mbali mbali za maisha na lengo kubwa ni kuondoa umasikini ambao upo kwao na familia zao. Kwanini nasema kwao na familia zao, nasema kwao na familia zao kwasababu, kijana hawezi kuwa masikini kama familia yake ni matajiri, la hasha, ila kwakuwa familia ni masikini basi hata kijana anauvaa umasikini ule uliopo katika familia, kwahiyo vijana wanapambana kutoa gamba la umasikini kwake na familia yake.

Kwa kawaida vijana wengi wamekuwa wakifanya shughuli nyingi za kuajiliwa na baadhi wamejiajili na waliojiajili ni wachache kuliko walioajiliwa katika sekta tofauti za kiserikali na za kibinafsi.

Vijana wanakwama wapi? Kwa namna vijana wanavyopambana tunatarajia kwamba vijana wamiliki Zaidi kuliko wale ambao si wa pambanaji kama wao, lakini unaweza kushangaa kwamba watu wazima ni watu wanaomiliki ukilinganisha na vijana.

Kuna mahali vijana wanapokwama na hapo ndipo ambapo watu wazima wametupiga hatua na kutuacha nyuma (lakini sio watu wazima wote).

Niliwahi kukutana na swali hili kwa wazee kadhaa

 Swalimbona bijana wasasa ni wavivu na hawana hata viwanja wala nyumba?”

Ukweli nilimuangalia sana huyo mzee na sikumpatia jibu kwa haraka, ila ilibidi nousome mtazamo yake kuelekea hilo swali, basi nilimjibu na kumuuliza swali

Jibu:hapana, vijana si wavivu isipokuwa wewe unawaona kuwa ni wavivu kulingana na vitu unavyomiliki, ukweli ni kwamba vijana wanapambana sana isipokuwa changamoto ni ugumu wa upatikanaji wa pesa na vyanzo vizuri vya uhakika wa pesa na hii inapelekea vijana kuonekana wwavivu wasio na kazi, kuhusu swala la viwanja, baba nilazima uzipime nyakati na uelewe nyakati pia, miaka ya 80 viwanja mtu ulikuwa unajipimia kwasababu maeneo yalikuwa wazi lakini kwasasa maeneo mengi yameshakaliwa na watu yamekuwa na thamani kulinganisha na nyakati zenu, miaka yenu mtu kumiliki Hekali 10 hadi 20 ilikuwa rahisi ila kwasasa ni ghari sana, vijana wanatafuta, usiwatazame kwa namna unavyowatazama, alafu usilinganishe 1950 na 2024 utapata changamoto kubwa kichwani kwako.”

Alijibu: “Ila ni kweli mwanabgu, kwasasa hali ngumu sana, poleni ila fanyeni yote kwa akili, wekezeni, ishini kwa kuwekeza”

Huu ni ukweli usiofichika kwamba maisha ni magumu na watu tunapambana, isipokuwa tunafeli sana katika kutumia akili na heshima na hofu katika vyote tunavyovifanya na kuvipata pia.

 Vijana Tunafeli hapa

1.       KUKOSA MAARIFA

Vijana wengi hatutumii akili katika kufanya mambo na hii ni kwasababu vijana tuliowengi hatupendi kujifunza isipokuwa tunapenda kujifurahisha.

Vijana wengi wa kitanzania sio wapenzi wa kusoma vitabu vinavyoelezea mambo ya mafanikio ila niwa taalamu wakusoma hadithi za mapenzi na post za mapenzi, badala ya kuwa busy kutafuta mambo yanayowasaidia kupiga hatua za kiuchumi wanapiga mbio kutafuta mambo yanayowasaidia kupiga hatua kwenye mapenzi. Sasa jambo hili linawapelekea waliowengi kushindwa kufanya mambo ya maana na hata pesa wanazozipata zinaishia kwenye mapenzi na mahusiano basi.

Mtu yuko radhi kununua Mkongo kwa Elfu 50 akamkomoe binti ila hayuko radhi kutumia elfu 10 kununua kitabu cha mbinu za mafanikio. Inachekesha lakini ndio uhalisia tulionao kwa vijana wa Tanzania.

Mbaya Zaidi kwasababu ya mapenzi vijana wanatoa hata pesa za mabosi zao kumpatia mwanamke (kuhonga) ili apate hata masaa 2 ya kufanya mapenzi naye kuliko kuitumia hiyo pesa kuwaza nmana gani nitaweza kuanzisha biashara yako.

Heshima kwenu wanachama Hai wa UWABATA (Umoja wa wanaume Bahili Tanzania). Mapenzi imekuwa ni changamoto kubwa inayoharibu ndoto na mpangilio wa maisha ya vijana wengi, ni upumbavu ambao umevitawala vichwa vya vijana wengi, ni mdudu uliotawala vichwa vya vijana wengi.

Vijana hatutumii akili naam hatutumii maarifa kwasababu hatuna hayo maarifa, na hatuna hayo maarifa kwasababu hatuyatafuti, ili kufanikiwa lazima kutumia akili na maarifa ya nyongeza kutoka kwa watu mbali mbali waliofanikiwa. Tafuta akili

2.       KUTOKUHESHIMU

Ndugu zangu, Vijana wenzangu na rafiki zangu pia, unajua kuheshimu ni kitu kikubwa sana, yani mtu kuwa na heshima ni jambo ambalo linaweza kukufanya wewe kufanikiwa, heshima sio kusema “Shikamoo….!!” Hapana ispokuwa heshima ni upendo/ nidamu ya ndani kwa mtu au kitu chochote kwa uwezo wake, ubora wake au mafanikio yake na na kuendelea. Kuwa ma heshima maana yake ni kuona thamani ya kile kitu na kukichukulia cha thamani, Heshima ndio kitu pekee kinachoweza kumfanya kijana afanikiwe.

Kijana anatakiwa kuheshimu kila mtu anayemuona, haijalishi anamfahamu au hamfahamu, kwasababu pesa zina watu na watu wana pesa, usipo waheshimu watu maana yake huna heshima na mahali pesa zilipo, huu ndio ukweli halisi.

Pesa inatakiwa iheshimiwe kwa kiwango kikubwa, yaani hata ukiwa na senti 1 unasababu ya kuiheshimu pesa na kuiona ya thamani, kwani pesa kwa kawaida ni ngumu kuipata lakini ni rahisi sana kuitumia.

Pesa unayoipata ukiiheshimu, lazima uitumie wa nidhamu, matumizi mazuri ya pesa yanategemeana na nidhamu kubwa uliyonayo katika matumizi ya Pesa hiyo. Vijana wa hovyo, hawaelewi nini Thamani ya pesa wakiwa nayo, wanaelewa thamani ya pesa wasipokuwa nayo. Huu ni upumbavu uliokithiri.

Kwasababu ya watu wengi kutokuheshimu pesa basi inafikia kuwasema vibaya vijana wenzao waliofanikiwa kwa kuwapa majina kama mafrimason na kadhalika, lakini hawajui namna gani walivyohangaika hadi kufikia hapo walipo. Vijana hawaheshimu pesa na hawaelewi faida ya kuheshimu pesa, mwisho wa siku umasikini unawatawala. Siku zote utakacho kiheshimu kitakuheshimu, ukiiheshimu pesa nayo pia itakuheshimu.

3.       KUPOTEZA KUMBUKUMBU

Vijana tuliowengi huwa tunapoteza kumbukumbu ya wapi tulipotokea na wapi tunapoelekea, na hii inatufanya tuwe vijana tuliochanganyikiwa, kumbukumbu ni kitu kinachoweza kumsaidia mtu kujielewa yeye ni nani, kutokuwa na kumbukumbu kunapoteza kabisa uhalisia wa kijana kuishi katika ndoto yake na hatimae kuwa bendela fuata upepo, kumbukumbu ni msingi sana kuelekea mafanikio ya aina yoyote, Kwa kadri tunavyo vaa Crazy Jins ndivyo tunavyokuwa na Crazy Minds, ukuivaa crazy jins alafu na wewe hujielewi hujakpsea ukosahihi kwasababu ndivyo ulivyo. Usinielewe vibaya, nina maana hii, ukifanya kitu cha kijinga na mtu akidhani kwamba uko sahihi akasahau kwamba haukumbuki ulikotoka na wala hujui unakokwenda atakuwa haelewi kwamba jina la vazi linasadifu yaliyomo.

Iko hivi, kumbuka wapi ulipo na wapi unapoelekea, ni rahisi sana wewe kufanikiwa kwenye maisha yako endapo utakuwa angalau na kumbukumbu ya maisha yako na hatima yako wewe na familia yako, na hapa utaheshimu kile kidogo unachokipata na utakiona kuwa cha thamani sana Zaidi ya mambo yoyote, unaweza kumkuta mtu anakwambia maisha magumu, ukimuuliza kwanini atakwambia pesa ngumu, ukimuulia kwani unampango gani na pesa, utakutana na majibu ya ajabu ajabu. Vijana Hatujitambui.

4.       HATUHESHIMU MUDA

Kwa kutokujua thamani ya muda tulionao wengi wanaamini watapata kesho, na hiyo kesho inaandaliwa lini? Sijui, huu ni ujinga ambao asilimia kubwa ya vijana tunao, na tunasema tutapata kesho alafu hatuna kitu tunachokifanya leo kitakachotupa faida kesho, Tunasubiri Mungu atujalie tufanikiwe, sikia rafiki, hata waliokufa masikini pia walikua wanasali, wanafunga na wanaomba sana naam Imani haiwezi kuzaa matunda kama anaye amini hajishughulishi, ndio maana hata maandiko yanasema “Mungu anazibariki kazi za mikono yako” Ayubu 1:10 “kazi za mikono yake umezibarikia. Nayo mali yake imeongezeka katika nchi” aiseee Mungu anambariki anayefanya kazi tena sio kazi kwa mikono tu na awe na akili, usipokuwa na akili huwezi kufanikiwa hadi unakufa. Heshimu muda ulionao, fanya mambo kwa ratiba na muda hapa utafanikiwa kwa nafasi kubwa sana,

5.       HATUNA MALENGO

Swala la kuwa na malengo ni changamoto sana, vijana wengi tunamalengo lakini sio malengo hai, tunayomalengo ambayo yapo tu na yatafanikiwa kwa mpango wa Mungu sio kwa jitihada zetu kuyatimiza. Kuwa na malengo ya namna hii ni sawa tu na mtu asiye na malengo yaani unaishi ishi tu kuendana na chochote kitakachokuja, Kijana una kila sababu za kujiwekea malengo yako, chochote kitakachokuja nje ya malnego yako maana yake ni kwamba sio kitu sahihi kuwepo upande wako, hivyo kipige chini kisha endelea na mambo meninge maana hicho hakikufai kabisa. Naongeza kusema panga malengo, weka malengo, simamisha malengo hapo utafanikiwa

6.       HATUYAISHI MALENGO

Swala la kuwa na malengo na swala la kuyaishi malengo, ni maswala mawili tofauti, unaweza kuwa na malengo lakini usiweze kuyaishi hayo malengo, vijana tuliowengi tunafeli kwasababu tuna malengo ambayo hatuyaishi, ukiwa na malengo hakikisha unayaishi yaani unayafuata, yanakuongoza  chakufanya ili kuyafikia, ukishindwa kuyafuata malengo yako basi hauna maana ya kuwa na malengo, kuyaishi malengo ni jitoa sadaka, yani kubali kuacha kila kitu na ufanye swala linaloleta mafanikio ya malengo yako, panga kufanikiwa, alafu yatafute mafanikio.

HITIMISHO.

Maisha ya ujanani ni maisha yenye changamoto nyingi, lakini ni mahali pekee unapoweza kutengeneza kesho yako iliyo nzuri na ya kuheshimiwa na kukumbukwa na watu. Wekeza muda wako katika kufanya na kuwaza mambo yenye tija na maisha yako, mambo yasio na faida achana nayo na utazame tu ulipo na unapoelekea. Najua ukiishi kwa kufuata ndoto zako kufanikiwa lazima.

Unaswali lolote?

Usiogope, comment hapo chini na nitakuja kukujibu kwa wakati

Naitwa THOBIAS COSMAS ukipenda niite Caza von Th. Cognitiologistic

About TECHNO ONLINE RICHES

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

1 comments:

  1. Hahahahahaaaaaa dahh nimebidi nicheke kwanza, ila umefundisha na umeelekeza vyema, bado nitakuwa na swali baadae maana huo ushauri ni kuntu

    ReplyDelete