10 DAYS MISSION STORY INAYOTARAJIA KUFANYWA NA CAZA MEDIA

 10 DAYS MISSION

OPENING SCENE

Inaonekana sehemu ambayo inamchanganyiko wa mazingira yenye miti na yasiyo ya miti, na mahali hapo pamejichora kwa mwanga mweupe kama mlango mara anaonekana Thoanson akiifika mahali hapo na mwili wake tayari ulikuwa ukiwaka nuru kuendana na mazingira hayo na mazingira yote yalionekana kubadilika rangi kuendana na rangi ya vazi alilokuwa amevaa. Wakati akiwa anazidi kuyasogelea hayo mazingira ndipo sauti ilisikia nyuma ya Leanh ikisema

Leahn:                         don’t go please, don’t leave me (huku akilia kwa uchungu na akikimbia)

Thoanson alisimama na kugeuka kumuangalia huku akidondokwa chozi na  Leahn alifika na kumkumbatia na Thoanson alimwambia

Thoanson:       I’m with you ever , I’ll be here again, wait me here.

Basi Thoanson alijitoa mkononi mwa Leahn na alianza kusogelea ule mlango na mara aliyeyuka, Leahn alisogelea mlango na mara ulipotea. Alikosa cha kufanya na kuanza kulia katika mazingira yale na mazingira yote yalibadilika na kuwa katika hali yake ya kawaiada.

 

SCENE 1

Ni majira ya usiku Wanaonekana vijana watatu wakiwa wamevaa wote mavazi ya suti wakielekea sehemu moja pa nyumba ya zamani vijana hao ni Thoanson, Reggan na Jackpol. Vijana hawa waliingia hadi katika nyumba hiyo na mara walihisi kama kuna mtu yuko nyuma yao. Wote macho yao yalibadilika na rangi za mavazi yao zilianza kutand kwenye mazingira yale na ndipo Mr. Colin aliposema huku akitembea kuwafuata

Mr. Colin:        ujio wenu niliutegemea kitambo sana, karibuni nyote makazini kwenu mlipopaacha kwa miaka mingi sasa.

Alipoongea hayo basi wote walitulia na kila kitu kilirejea mahali pake na ndipo mr. colin alipoenda kukaa huku akigusa ndevu zake ambazo zilionekana nyeupe sana. Alimuita

Mr. Colin:        Pandora is like abandoned palace, marooned survive within the jungle

Walimtazama wote kisha walimsogelea alishika mawe matatu mkononi mwake nay ale mawe yalianza kutoa mwanga mweupe wenye mchanganyiko na blue na baada ya hapo basi anga lilianza kupiga radi na wale watatu walinyosha mikono yao kuyaelekea yale mawe na ndipo kila moja alipokea jiwe moja kutoka mikonono mwa Mr. Colin kisha alisema.

Mr. Colin:        a hundred of years am waiting you, now let’s live as an equal

Baada ya maneno hayo mawe yaliyeyuka mikoni mwao na waliondoka pasipo kuongea kitu.

 

SCENE 2

Ni majira ya asubuhi wanaonekana Thoanson, Reggan na Jackpol wakitembea huku wakizungumza

Reggan:           Tumebakiwa na muda mchache sana n ahata hivyo bado sielewi ni kwa namna gani tunaweza kulimaliza kwa wakati jambo hili

Jackpol:           yote yanawezeekana cha msingi tupambanie kinacho tuhiusu kwa wakati tu, au unasemaje Thoan, thoan aliwajibu kwa kutikisa kichwa tu kisha mbele yao alitokea ghafla binti aliyekuwa anakimbizwa na watu anaonekana alikuwa mwanafunzi na hao walikuwa wanafunzi wenzie na ndipo alipompamia Thoanson alipompamia, Thoan alikasilika na kumuinua yule bint huku akiwa amemkazia macho kwa hasira. Reggan na Jackpol waliangaliana na kisha wakamshika mkono Thoanson na wale vijana waliposogea karibu na Leahn walisema Tyler, Posey na Morgan (mikononi mwao walikuwa na magongo)

Tyler:               nyie akina nani mlie kaa katika njia zetu

Thoanson, Reggan na Jackpol walikuwa wakiwatazama tu na Leahn alikuwa akiwaomba msaada.

Posey:             alinyanyua gongo na kumyoshea Leahn, You  are our meet today, you have no way to escape.

Leahn alijificha nyuma ya Thoan na ndipo Jackpol aliposema

Jackpol:           Very sorry guys, allow us to go coz……. we don’t want to hurt anybody here

Morgan:          you fuck let kill brats

Wakati wakitaka kuwakaribia mr. colin alitokea na kuwanyang’anya yale magongo na walishangaa hawana kitu tena mkononi na vipo mikononi kwa mr. colin.

Mr. Colin:        you small brats, leave now alimgeukia Leahn na kumwambia Just go you are safe now

Leahn aliinamisha kichwa ishara ya kuwashukuru kisha aliondoka na kuelekea nyumbani.

 

SCENE 3

Ni majira ya usiku anaonekana Leahn akiwa anajisomea na mara ghafla aliacha kusoma na kukaa huku akipiga piga peni kwenye meno ishara ya kuwaza na alikuwa akiwakumbuka wale vijana aliowagonga pale njian wakati anatoka shuleni, alikuwa akikumbuka anaishia kutabasamu na ndipo mama yake alimuita Miss Choi

Ms. Choi         Leahn mwanangu, njoo chakula tayari

Leahn:                         ahsante mom, nakuja

,eahn alitoka hukua akionekana mwenye furaha na alimkuta mdogo wake amekaa mezani na mama yake akiwa kama mwenye usingizi anasinzia sinzia, kwa furaha alifika na kuanza kupitisha mkono karibu na uso wake, akaona hastuki kisha akamnong,oneza amkaa lakini bado hakuamka na ndipo alipomshtua kwa sauti heeeeeeee alishtuka kwa sauti na ndipo mama alipogeuka kumuangalia Leahn

Miss Choi:       hukui tu?

Dylah:             Mama lakini umemuona dada aaahh (analalamika kwa kudeka)

Leahn alisogea na kumkumbatia mdogo wake na kumwambia

Leahn:                         am sorry dada, sorry haya tule sasa akaanza kumlisha

Mss. Choi:       leahn mbona leo unafuraha sana mwanangu what’s on?

Leahn:                         aa hamna kitu mom, ni hali tu ya siku

Ms. Choi:         okay

Basi waliendelea kula na ndipo kwa muda kidogo Leahn alianza kucheka mwenyewe na mama alimuangalia na kutikisa kichwa.

 

SCENE 4

Ni majira ya asubuhi wanaonekana Miss Choi na Ms Lidya wakiwa ofisini kwa mwalimu wa darasa akiongea nao kuhusu matukio yanayofanywa na ilikuwa ni baada ya watoto wao kuonekana kuwa na changamoto pale shulen

Mr. Thomas    Ms Lidya na ms choi, kuna nini kinachoendelea kwa watoto wenu mbana kama wanaugomvi sana na mara nyingi ninakutana na taarifa za watoto hao

Ms. Lidya        no sina taarifa yoyote kama kuna jambo linaloendelea kwao

Ms. Choi         unajua ni jambo geni pia nalisikia, kwani kuna nin?

Mr. Thomas    Morgan anakikundi chake wakiwa watatu posey na Tyler, wamekuwa kikwazo sana kwa watoto hapa shulen na inasemekana wanamsumbua sana Leahn kwahiyo nachotaka kuwaomba ni kwamba hususani kwa Miss Lidya, muonye mwanao na kundi lake maana imekuwa ni tatizo hapa shuleni

Ms Lidya         ahsante  mwalim nitalishughulikia swala hili

Mr. Thomas:   wewe unaweza kwenda nibaki na madam choi. (alinyanyuka na kuwaaga kisha aliondoka) akasema

Mr. Thomas    tafuta namna ya kumsaidia mwanao ili awe salama la sivyo inaweza kumgharimu sana katika masomo yake, na hili jambo nakwambia kuwa wale vijana ni wahuni tena wababya mno. Kuwa nao makini.

Ms Choi          sawa haina shida lakin pia naomba uwe mliznzi pia kwake maana mm mara nyingi niko mbali nae.

Wakati huo anatoka nje madam lidya alimkuta Morgan amekaa na rafiki zake sehemu na ndipo posey alipomuonyesha mama yake morgan aligeuka na kumuona kisha alinyanyuka na kumfuata

Morgan:          vipi mama mbona huku tena saiz

Ms. Lidya        unapokwenda mahali fanya ulichokifuata yasiyokuhusu achana nayo {kwa ukali}

Morgan alimuangalia mama yake pasipo kumuelewa na alionekana kuchoka na mama yake aliondoka. Na ndipo Morgan aliporudi kwa rafiki zake.

 

SCENE 5

Ni majira ya usiku inaonekana nyumba ikiwaka moto na nje ya nyumba alionekana Mr. Ronelt akiangalia yote yanayoendelea na moto ule ulikuwa ukiambatana na rangi ambazo hazikuwa za kawaida, na wakati huo huo alionekana mtu akitoka maeneo ya nyumba hiyo inayowaka moto na alipotoka nje Mr. Ronelt alinyosha mkono na yule mtu alijikuta ameshafika karibu na mr. Ronelt. Mr Ronelt alicheka akazungusha mikono yake kisha kikatokea kitu mkononi mwake alimfumbua mdomo yule mtu na kumlisha baad ya alimuacha chini yule mtu maana alikuwa ameungua kisha alinyanyua mikono juu na kuondoka kwa kuchukulia na miale ya blue na yule mtu alibaki pale

Upande wa pili MR. colin aliona jambo lile n ahata upande mwingine walipokuwa wamekaa nje Thoanson na wenzie waliona jambo lile na walijua kuwa kuna tatizo tayari. Na ndipo Thoanson alisema

Thoanson:      ronelt ronelt ronelt, aliposema hivo upepo mkali ulivuma na sauti ilisikika (Remember your duties)

Wote walitikisa kichwa kwa ishara ya kupokea neon hilo.

 

SCENE 5

Ni majira ya asubuhi anaonekana Locky akiwa amelala hospital na mwili wake ukiwa umeungua vibaya na moto, na wakati huo alikuwepo nesi Judith akiendelea kumuhudumia, wakati anatoka alikutana na Mr. Thomas, na Thomas aliingia na kufunga madirisha yote kisha alijibadili na kuwa Mr. Ronelt, alisema

Mr. Ronelt      ni wakati wa wewe kuamka maana tayari imetosha kulala kwako, alisogea na kukaa kitandani kisha akasema, you are now a man from Pandora

Ghafla alihis kama kuna mtu anakuja na alirudi kwenye umbo la mr. Thomas kisha aliingia nesi na yeye aliamua kuondoka na ndipo nurse Judith alipokuwa anaweka dawa cha ajabu anasikia kama mtu anaongea kugeuka kumuangalia Locky ngozi inajirudisha kwenye hali yake oohhh alipata kiwewe na kuaguka chini. Locky alinyanyuka na kukaa kisha alichomoa drip na alinyanyuka akiwa mzima wa afya kabisa. Jambo la ajabu ni kwamba Locky hakuwa na kumbukumbu ya aina yoyote isipokuwa alikuwa na neon moja, alipofika nje ya hospitali alimkuta Ronelt amemsubiri kwenye gari na aliondoka naye

 

SCENE 6

Wanaonekana Posey, Tyler na Morgan wakiwa wameshika magongo kama kawaida yao wamemzunguka Leahn pamoja na rafiki yake Suzan, huku wakilia kwa woga mara walianza kusikia kama upepo ukivuma na ndipo walijikuta wote wako chini, isipokuwa Suzan na Leahn. Walipojikuta chini basi Leahn na Suzan walikimbia na walipoondoka ndipo Thoan, Reggan na Jackpol walipotokea mahali kusipojulikana kama upepo, miili yao ilikuwa inawaka mwanga mweupe mchanganyiko na blue na akina morgan waliogopa sana na kukimbia wote

 

SCENE  7

Wanaonekana Thoanson, Reggan na Jackpol wakipeana mikakati majira ya usiku

Thoanson;       Tulipewa siku 10 na sasa tumebakiwa na siku saba tu inatakiwa turudi nyumbani, na kwasasa nilitamani kila mmoja apambane kwa nafasi yake, kwakuwa wote tunalengio moja basi kila mmoja afanye kwa upende wake ili tulifanikishe hili swala kwa wakati

Reggan:           yeahh wazo zuri kiongozi, nadhani tuliishi wazo hilo ili mambo yawe sawa

Jackpol:           kweli, okay sasa, ninawazo pia katika hili jambo, mr. Thoan nadhani wewe ungekuwepo pande za chuon maana yule mtu aliyeungua na akawarestored anasoma pale na tayari anayonguvu ya tofauti kidogo kwahiyo, hakikisha wewe unaingia shuleni kwa namna yoyote.

Thoan:             sawa haina shida juu ya jambo hilo, na pia nyote mjigawe tutakuwa tukikutana mahali hapa kuona wapi tumefikia na wapi tunaelekea.

Reggan;           sawa, tufanye kazi

 

SCENE 8

Ni majira ya mchana anaonekana Mr. Thomas Lee akimtambulisha mwalimu mpya katika darasa la Leahn na posey na kundi nzima na alisema

Mr. Thomas:   hello!

Students:        Yes sir

Mr. Thomas:   we have got a new teacher who will help in scientific field and imaginative life, so, receipt him.

Mr. Thoanson my name is Thoanson Thobias ahmmmm I need you cooperation, thank you

Baada ya kuongea hayo basi walitoka.

 

SCENE 9

Baada ya muda mchache, Wanaonekana Morgan na kundi lake wakimjadili mwalim, walisema

Morgan:          huyu jamaa si alikuwa siku ile na wenzie watatu wakatuzuia hao tusimpate Leahn

Posey:             ndiyo yeye hata hujakosea, lakini acha tumuonyeshe maisha yakoje, si amejileta mwenyew

Morgan:          dogo (huku akimgusa bega tyler) hakikisha anaingia 18 zetu

Tyler:               jambo dogo hilo ngoja tumfanyizie

 

SCENE 10

Anaonekana Reggan akiwa katika mizunguko yake majira ya asubuhi na alikutana na Miss Lidya akiwa amekaa na Locky na walikuwa wakizungumzia namna gani ajali ilivyotokea pale, na ndipo alipowasogelea na kuanza kuzungumza nao kwa upole

Reggan:           habari, samahani sana kwa kuwavurugia mazungumzo yenu.

Locky alimuangalia kuanzia juu hadi chini na miss Lidya alisema

Ms Lidya:        karibu ukae wala hata usijali

Reggan alisogea na kukaa kisha aliuliza.

Reggan:           samahani naomba kuuliza! Namtafuta ndugu yangu anaitwa Ronelt sijui mnamtambua! Nimepotezana naye Zaidi ya miaka 10 sasa, tafadharini kama mnamfaham naomba mnisaidie

Katika swala hilo Locky alimuangalia sana Reggan kwa kumtamani  na Reggan aligeuka na kumtazama locky alivyokuwa akimuangalia alipotezea kisha alisema

Reggan:           inasemekana kwamba yupo katika mji huu na ndio maana nimekuja kumtafuta

Ms Lidya:        hapana kwa mitaa hii bado sijaisikia jina hilo lakini tutapeana taarifa pindi atakapoonekana

Reggan:           ni muhim sana kuonana nae Napata wakati mgum sana juu yake

Locky:             hatumfaham elewa basi brother

Reggan:           okay sawa, nashukuru sana na mnisamehe sana kwa usumbufu.

Reggan alisimama na kuondoka na ndipo Locky alipomtazama kwa kumtamani na ms Lidya alisema

Ms Lidya:        vip kwan una Ideal na huyo Ronelt

Locky alimjibu huku akinyanyuka na kusema

Reggan:            sina Ideal nae

 

SCENE 11

Ni majira ya usiku, Wanaonekana Ronelt na Locky wakiwa wanaongea kuhusu reggan ambaye alionekana kumuulizia sana

Locky:             unafuatiliwa na kijana mmoja ila nilipomuangalia vizuri hakuwa mtu wa kawaida

Ronelt:             oohhh kumbe (huku anatikiswa kichwa) sawa, nimekuelewa, hatuna haja ya kuizungumzia hiyo mada, isipokuwa unakazi moja ambayo unatakiwa kuifanya kwa wakati huu

Locky:             nakusikiliza kiongozi

Ronelt:            vizuri fumbua macho yako kisha nitazame mimi

Basi lock alimuangalia kwa kumkazia macho na ndipo nguvu ya mwanga kama wa blue ulitoka ndani ya macho ya ronelt na kuingia kuonekana ukielekea kwa Lock, Lock alisikia kama maumivu na ndipo alipojikuta kama kazingirwa na kitu kama ukuta ambao ni transparent wenye rangi za mg’ao. Basi Ronelt alitabasam na ukuta ole na hali ya hewa ilitulia na ndipo alipotoka kama anaondoka na mkononi mwake alikuwa ameshika jiwe, alirusha lile jiwe kumuenedea lock na lock alipoikazia macho basi ile jiwe iligandanda mbele ya uso wake na moto uliwaka kwenye lile jiwe na likapasuka.

Baada ya hilo alisema

Ronelt:            Nenda kawaangamize hao wako watatu, fanya majukumu yote kama ninavyokuagiza mimi.

Locky alitikisa kichwa kwa ishara ya kukubali kisha ulionekana moto ukimzingira na kupotea nae Ronelt alichukuliwa na wingu jeupe.

 

SCENE 12

Majira ya mchana, Anaonekana Jackpol akiwa kwa mjomba Mr. Colin ndani kwa mr. colin, alikuwa akizungumza nae ndani kuhusu mambo yanayo fanywa na Ronelt

Mr. Colin:        Ronelt anafanya mambo mengi maumivu anayaacha kwa watu wengi, tumekuwa tukishindana kwa muda mrefu sana mimi nay eye japo nilikuwa nikiwasubiri kwa ham maana nilijua lazima mrudi ili mje kukamilisha kisasi mlichonacho juu yake.

Jackpol:           samahani Uncle, umesema kisasi?

Mr. Colin:        hapana umesikia vibaya, nimesema kwakazi sio kisasi (huku akijiumauma)

 

Jackpol aligeuka na kumuagalia kwa mkazo kisha akasema

Jackpol:           unanificha nini uncle? Kwani Huyu anahusika nini na mimi hata unazungumzia kisas? Nambie ucle whats on?

Mr. Colin:        cool down, nothing, just stay humble and cool. Nilikuwa sijamalizia story, au ngoja nikakuletee kwanza chakula najua hujala tangu asubuhi, kaa hapo nisubiri

Mjomba alisimama na ndipo Jackpol alipoingia ndani ya dimbwi zito la mawazo kwa habari aliyoisikia ya kisasi

 

SCENE 13

KUMBUKUMBU

Inaonekana nyumba Ikiungua na sauti za watu mama na mtoto zikisikika ndani na ndipo nje anaonekana mtoto akija haraka alipokuta hali ile moto umetandana mahali kote alilia na kupoteza faham, na ndipo alipoonekana mtu akitaka kumchukua na mtu (Mr. Ronelt) huyo alitokea kwenye moto kule, pindi tu alipotaka kumgusa mara kitu kama mshale wa moto ulipita mkononi mwake na kumbe Alitokea Mmmoja kati ya viongozi wa Pandora camp na kumzuia asimchukue yule mtoto, alipogeuka na kumuona aliamua kukimbia kwa kuyeyuka ndipo yule kiongozi Scott alipounganisha mikono yake kifuani mwa mtoto na mwangaza uliwaka mikononi mwake kisha aliondoka na mtoto.

 

SCENE 12 CONTINUITY

Baada ya kukumbuka tukio hilo bas hasira ziliongezeka kwa Jackpol na kuanza mabadiliko ya hali ya mazingira ya mwili wake kwa kuwaka kama moto wa blue.

Mjomba alirudi na kumuangalia sana kwa makini kisha alisema

Mr. Colin:        usijekufanya kitu ukiwa na hasira itakugharimu sana, acha hasira, najua umesha ujua ukweli basi tulia.

 

SCENE 14

Wanaonekana Thoanson akiwa na Leahn wakiongea ofisini na

Thoanson:       Leahn unatatizog gani na kundi la morgan

Leahn:                         ukweli binafsi sina tatizo lolote na wao, isipokuwa Morgan aliwahi nitaka kimapenz nikamkatalia ndio tokea hapo amekuwa na vita na mimi, kwahiyo vitailiyopo kati yetu ni ya mapenzi tu hakuna jambo linguine.

Thoanson:       na vipi wazazi wako wanalifaham hili jambo?

Leahn:             hapana sijawahi kuwajuza juu ya jambo hili, kwahiyo sina Imani kama wanalitambua

Thoanson:       sawa, kuwa makini nao, maana hawana nia njema na wewe, infact, just go and another time nitakuita sawa!

Leahn:                         sawa nashukuru

Basi Thoan aliendelea na majukum yake

 

SCENE 15

Ni majira ya asubuhi, Anaonekana Locky akiwa chuoni pamoja na wanafunzi wengine na hakuwa mwanafunzi, baada ya muda akiwa darasani alikuwa makini katika hali ya utulivu na kugundua kuwa kuna mwanafunzi mmoja aliye kuwa kinyume na Thoanson, baada ya darasa alitoka nje na alimuita Morgan, Morgan alimfuata na kumwambia

Locky:             nataka nikupe kazi moja unifanyie kwa wakati

Morgan:          kazi gani wewe tunasumbuana

Locky:             tulia dogo, usije ukaumia sawa,

Morgan;          kwo unanitisha nini? Alafu sikia siogopagi wajinga kama wewe, nitakugeuza bucha chap

Locky:             (alitabasamu kwa dharau) achana na hayo, nataka uniambie huyu Thoan anashida gani na wewe, nataka nikusaidie

Morgan:          Bwana Mambo yangu hayakuhu, wewe fuata yako (kwa dharau)

Locky alikasirika na kumbana ukutani huku macho yakiwa yamebadilika rangi alimshika shingoni kwa mkono wa kushoto na kumnyanyua kwa mkono mmoja kisha akamwambia

Locky:             jambo gani linaloendelea kati yenu

Morgan:          (kwa uoga na maumivu alisema) ananiingilia kwenye mapenzi

Locky:             (alimuachia na kumwambia ) uwe na adabu, mpenz wake anaitwa nani?

Morgan:          Leahn

Locky alicheka na kumnyoshea dolr gumba akimanisha poa kisha aliondoka, Morgan alimuangalia sana na kuogopa mno.

SCENE 16

Anaonekana Locky akiingia chumbani mwa Morgan usiku na morgan alikuwa amelala, na Lock alimuita Morgan, Morgan alishtuka na kumkuta lock aliogopa sana na kuanza kumuuliza Morgan:            umefuata nini?

Locky:             nimekumiss (huku akitabasam)

Akimukazia macho morgan aliogopa na Lockky alimwambia, nitazame

Alipomtazama basi Lock alimwambia nakupatia zawadi, nenda kamshinde adui yako ili umpate umpendae sawa.

Morgan alitikisa kichwa ishara ya kupokea neon lile kisha macho ya Locky yaliwaka na nuru ile iliingia kwa Morgan na ndipo morgan alipopiga kelele za maumivu maana alisikia kama moto unawake ndani yake, mama yake alisikia na alikuja haraka hadi kwa morgan, alimuuliza.

Ms. Lidya:       kuna nini Morgan

Morgan:          hakuna tatizo mama, na wakati huo Locky alikuwa kashaondoka.

 

SCENE 17

Ni majira ya usiku wanaonekana Thoanson, Reggan na Jackpol wakiongea kuhusu walipofikia lakini Jackpol alikuwa na hasira mno kulingana na kwamba tayari alijua chanzo cha matatizo yaliyoikumba familia yake

About TECHNO ONLINE RICHES

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment